
MAKUNDI ya upinzani nchini Syria yanayokutana mjini Doha, yamekubaliana
kimsingi kuhusu mpango wa umoja dhidi ya rais Bashar al-Assad.
Washiriki
wa mkutano huo wamesema ambapo watakutana leo.
"Tumekubaliana kuhusu vipengee viwili juu ya kuundwa kwa muungano wa
kitaifa nchini Syria kwa ajili ya majeshi ya upinzani na mapinduzi.
Tutaendelea na majadiliano yetu kuhusu mambo yanayohusika katika
muungano huo leo Jumapili," mmoja wa viongozi wa muungano huo wa
upinzani Suhair Atassi ameliambia shirika la habari la AFP baada ya saa
12 za mazungumzo.
Kiongozi mpya wa SNC George Sabra.
"Tulikuwa katika hatua ya kutia saini makubaliano lakini tumeonelea
kutoa muda zaidi ili kutathmini sheria za ndani kwa ombi la baadhi ya
makundi," amesema mjumbe mwingine Riad Seif, ambaye anaripotiwa kuwa
anaonekana na serikali ya Marekani kuwa ana uwezekano wa kuwa mkuu mpya
wa upinzani.
NSC lakabiliwa na mbinyo.
Washiriki walitarajiwa kurejea katika mazungumzo leo asubuhi. Mkutano
huu unakuja baada ya baraza la taifa la Syria SNC kukabiliwa na mbinyo
kutoka kwa mataifa ya Kiarabu na mataifa ya magharibi kukubali mpango wa
umoja wa upinzani, huku kukiwa na hali ya kukata tamaa miongoni mwa
makundi ya wapiganaji.
Hapo nyuma likiwa linatambulika kama wawakilishi wakuu wa upinzani
lakini kadiri ya muda ulivyokwenda lilipoteza hadhi hiyo katika serikali
ya Marekani , kutokana na kudhibitiwa na watu ambao wanaishi uhamishoni
na hawana uhusiano wa karibu na hali halisi ndani ya nchi, baraza hilo
la SNC , lilitakiwa mara mbili kuahirisha mazungumzo juu ya mpango wa
kuunda serikali itakayojumuisha makundi mengi ambayo itakuwa inasubiri
kuchukua madaraka ndani ya Syria.
Makubaliano hayo yako katika msingi wa harakati zinazochukuliwa na Seif
ambazo zina lenga kuundwa kwa serikali ya mpito , ambalo ni baraza la
kijeshi litakaloshughulikia makundi ya waasi ndani ya Syria na mahakama
ambayo itafanyakazi katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Mjumbe muhimu wa mkutano wa Syria mjini Doha Riad Seif
Serikali ya mpito
Serikali ya mpito ambayo itakuwa na wajumbe kumi itachaguliwa na kundi
jipya lenye wajumbe 60 ambalo litatokana na wanaharakati wa kiraia na
wapiganaji waasi ndani ya Syria, pamoja na wale wanaoishi uhamishoni
ambao wamedhibiti baraza la SNC.
Jana Jumamosi (10.11.2012) baraza la NSC limewasilisha pendekezo lake na
kiongozi wake mpya George Sabra amewaambia waandishi habari mjini Doha
kuwa baraza hilo la NSC ni la muda mrefu zaidi kuliko harakati nyingine
zozote, akiongeza kuwa makundi ya upinzani hayapaswi kulazimishwa kuwa
chini ya chombo chochote kingine.
Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Kwa mujibu wa shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria ,
zaidi ya watu 37,000 wameuwawa tangu vuguvugu la harakati za kuuondoa
utawala wa rais Bashar al-Assad kuzuka Machi 2011, harakati hizo
zilipoanza kwanza kama vuguvugu la amaandamano na kisha kugeuka uasi wa
mapambano ya silaha.

0 comments:
Post a Comment