Mkuu wa zamani wa huduma za intelijensia nchini Sudani Salah Gosh.
WATU 13
wakiwemo maafisa wa jeshi na wa serikali wanashikiliwa nchini Sudani kwa
madai ya kuhusika na mpango wa kuhatarisha amani nchini humo akiwemo
aliyekuwa kiongozi mkuu wa muda mrefu wa huduma za kiintelijensia
jenerali Salah Gosh.
Waziri wa habari nchini humo Ahmed Bilal Osman amethibitisha
kushikiliwa kwa maafisa hao na kuwataja wengine kuwa ni jenerali Adil
Al- Tayeb wa kitengo cha taifa cha huduma za kiintelijensia na usalama,
brigedia Mohammed Ibrahim wa vikosi vya kijeshi vya Sudani.
Waziri Osman ameongeza kuwa wote waliokamatwa wanachunguzwa kuhusiana
na mpango wa kuvuruga amani ambao awali ulipangwa kutekelezwa Novemba
15 lakini ulicheleweshwa hadi leo Alhamisi ambapo kitengo cha huduma za
kiintelijensia kimearifu kuwa kimefanikiwa kuharibu njama hizo.
Kwa upande wa msemaji wa muungano wa vyama vya upinzani amekanusha
kuhusika kwao katika jaribio la kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa njia ya
vurugu katika taifa ambalo limeshuhudia mapinduzi ya kijeshi saba au
majaribio ya mapinduzi katika miaka 56 ya historia yake.

0 comments:
Post a Comment