
VIKOSI vya usalama Misri leo vimeimarisha ulinzi mjini Cairo karibu na
uwanja wa Tahrir wakati wapinzani wakipanga kufanya maandamano makubwa
ya kupinga mabadiliko ya katiba yaliyoamriwa na rais Mohammed Morsi.
Ulinzi mkali umeimarishwa nje ya jengo la bunge, ofisi ya baraza la
mawaziri na karibu na makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani wakati
ambapo waandamanaji wakianza kuungana katika uwanja wa Tahrir.
Rais Morsi jana amesaini marekebisho ya katiba ambayo yanayompa kinga ya
maamuzi yake kutopitiwa na mahakama. Morsi ambaye amekuwa rais wa
kwanza wa Misri kuchaguliwa kiraia pia amembadilisha mwendesha mashitaka
mkuu ambaye naye aliteuliwa katika utawala wa sasa uliomwondoa
madarakani Hosni Mubarak.
Mamlaka mapya kwa rais
Rais Mohammed Morsi wa Misri.
Kanuni hiyo iliyotolewa jana inalipatia kinga bunge linaloongozwa kwa
wingi na chama cha kiislamu na kumpatia mamlaka mapya rais ambayo ndiyo
yaliompa nguvu za kumfukuza mwendesha mashitaka mkuu na kumteua
mwengine.
Kanuni hiyo inaeleza kuwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na rais Morsi
mpaka wakati wa uchaguzi mpya wa bunge hayapaswi kuingiliwa kisheria.
Kanuni hiyo mbali ya kuonekana kama ya kimabavu lakini pia inaelekeza kurejewa kwa mashitaka ya maafisa wa utawala
Kauli ya upinzani
Upinzani wameita amri hiyo kama ukiukwaji wa uhuru wa mahakama na kudai
kwamba inamkinga Morsi ambaye tayari anao ushawishi wa mamlaka ya
wabunge na nguvu za kidikteta.
Hatua hiyo ni kama inaonekana muhimu katika kulinda mapinduzi ambapo
chama cha rais Morsi cha udugu wa kiislamu na washirika wenzake wamesifu
amri hiyo wakisema ni ''Mageuzi'' na kuitisha maandamano makubwa hii
leo kwa ajili ya kumuunga mkono rais Morsi.
Hata hivyo upo ukosoaji katika utawala wa rais Morsi ambapo wale wasiokuwa waislamu wanalalamika sauti zao kutosikika.
Katiba ni kipengele muhimu katika kipindi cha nchini Misri katika
kuimarisha demokrasia. Uchaguzi wa bunge jipya hautakuwepo hadi hati
hiyo itakapokamilika na kupitishwa kwa kura ya maoni maarufu.
Kanuni hiyo inatoa muda miezi miwili zaidi kwa tume kumaliza kazi yake
ikimaanisha kwamba kazi ya kutengeneza rasimu inaweza ikafikia mwezi
februari na hivyo kusogeza nyuma uchaguzi mpya.

0 comments:
Post a Comment