
JESHI la Polisi mjini Cairo Misri wanasema wamegundua gengi la watu wanaouza
watoto ambalo linafikiriwa kuwa limeuza watoto wachanga 300.
Wauguzi wawili na daktari wa zahanati moja mjini Cairo ni kati ya
wale waliokamatwa, na polisi wanasema bado wanamsaka meneja wa zahanati
hiyo.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao wa matibabu
wamepasuwa waja wazito wasiotaka kuzaa, na kuwatoa watoto wachanga ambao
waliwauza kwa familia zisokuwa na watoto.

0 comments:
Post a Comment