
WAZIRI Mkuu wa Misri Hisham Kandil leo ameutembelea Ukanda wa Gaza na
kuahidi kuwasaidia Wapalestina kurejesha utulivu kwa kusitisha
mashambulizi ya Israel ambayo yameendelea licha ya ziara hiyo.
Waziri Mkuu wa Misri Hisham Kandil leo ameutembelea Ukanda wa Gaza na
kuahidi kuwasaidia Wapalestina kurejesha utulivu kwa kusitisha
mashambulizi ya Israel ambayo yameendelea licha ya ziara hiyo.
Wakati huo huo Wapalestina nao wamerudia wito wao kwa Umoja wa Mataifa
wakiutaka kuingilia kati mashambulizi yanayofanywa na Israel katika
ukanda wa huo.
Waziri Mkuu wa Misri Hisham Kandil akiwa Gaza.
Waziri Mkuu huyo wa Misri amewaahidi Wapalestina kuwa nchi yake
itafanya juhudi kuhakikisha inawarejeshea utulivu kwa kukomesha
mashambulizi ya Israel ambayo ameyaita kuwa ni ya kikatili.
Kandil amesema kuwa Misri haitasita kuongeza juhudi zake na kujitolea
ili kusitisha ukatili huo.
Kiongozi huyo ameyasema wakati akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kuitembelea hospitali ya Shifa iliyoko
Gaza City na kuwaona baadhi ya majeruhi wa mashambulizi ya hivi karibuni
yaliyofanywa na Israel.
Israel yakiuka ahadi ya kusitisha mashambulizi
Hapo kabla Israel ilitoa taarifa kuwa itasitisha mashambulizi wakati wa
ziara ya kiongozi huyo kama nchi yake ilivyoomba lakini hilo
halikuwezekana kwa mashambulizi yameendelea kufanyika.
Ndege za kivita za Israel zimelishambulia eneo la kaskazini mwa Gaza
asubuhi ya leo na kuwauwa watu wawili. Shirika la habari la AFP
linaarifu kuwa ndege hizo zilipiga mabomu kwenye kundi la raia katika
eneo la Nazila kaskazini mwa Gaza City.
Tukio hilo limefanyika muda mfupi baada ya Israel kulituhumu kundi la
Hamas kuwa limekiuka makubaliano ya kutofanya mashambulizi wakati wa
ziara ya Kandil.
Ziara hiyo ilielezwa kuwa itachukua muda wa masaa matatu na inatazamwa
kama hatua ya Misri kuonyesha mshikamano na kuliunga mkono kundi la
Hamas katika kipindi hiki kigumu.
Benjamin Netanjahu, Waziri Mkuu wa Israel.
Misri iliiomba Israel kusitisha mashambulizi wakati wa ziara hiyo na
Israel imekubali.
Afisa katika serikali ya Israel anasema kuwa
Netanyahu amekubali kusitisha harakati zote za kijeshi kwenye ukanda wa
Gaza kama Misri ilivyoomba.
Hata hivyo majibu hayo pia yanasema
kusitishwa huko kwa mashambulizi kutafanya kazi tu endapo Hamas nao
watafanya hivyo hivyo.
Misri inapinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza ikisema
hayakubaliki, wakati Marekani ikisema kuwa inatambua haki ya Israel ya
kujilinda na mashambulizi ya Hamas.
Hapo kabla Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alizungumzia mashambulizi ya nchi yake dhidi ya Gaza na kusema
Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na jeshi la nchi hiyo zinasema kuwa
tayari limeanza kuandikisha vikosi vya askari 16,000 kati ya 30,000
vilivyoamriwa kuwa tayari.
Nayo Mamlaka ya utawala Wapalestina imepeleka kilio kuhusu mashambulizi
hayo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likilitaka kuingilia
kati na kusitisha mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika ukanda wa
Gaza ikiwa ni siku moja baada ya Baraza hilo kushindwa kuchukua hatua
hapo jana.
Mwangalizi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour
ameliandikia barua baraza la usalama akisema kuwa kitendo cha Israel
kupeleka vikosi vya kijeshi vya ardhini ikiwemo vifaru magari ya silaha
karibu na mpaka wa Gaza kinasababisha wasiwasi wa hali ya juu na hivyo
wanahitaji zingatio la jumuiya ya kimataifa.
Jana Wapalestina 19 kati yao wakiwemo raia 12 na Waisrael 3 wameuawa
jana kutokana na majibizano ya mizinga ya angani. Kati ya raia 12
waliouawa huko Gaza sita ni watoto.

0 comments:
Post a Comment