Mahakama Kuu Tanzania.
MPANGAJI wa nyumba namba 608 iliyopo eneo la Sinza jijini Dar es Salaam, Diana Philibert (41) amefungua kesi ya madai ya zaidi ya Sh24.2 milioni katika Mahakama ya Nyumba ya Kinondoni dhidi ya msimamizi wa nyumba hiyo, Godfrey Lubomola.
Katika kesi hiyo, iliyofunguliwa na Diana kupitia wakili wake Sabasaba Mashiku, anaiomba mahakama iamuru alipwe kiasi hicho cha fedha kama fidia ya kung’olewa kwa mita ya Luku na Service line katika nyumba hiyo aliyokuwa amepanga.
Kubomolewa madirisha, milango na kuibiwa baadhi ya vitu vyake ikiwamo fedha taslimu Sh5 milioni, kompyuta aina la Laptop, simu ya mkononi na nyaraka zake mbalimbali.
Pia anaiomba mahakama iamuru alipwe Sh10 milioni kama fidia ya usumbufu, kukosa amani kwa kumuhofia kuwa muda wowote angeweza kwenda kumfanyia kitu chochote kibaya na kwamba adhabu nyingine mahakama hiyo ya Nyumba iiangalie itakayoiona inafaa.
Katika kesi hiyo, Lubomola anadaiwa kuwa Mei 12, mwaka huu, akiwa msimamizi wa nyumba hiyo inayomilikiwa na Redemta Kalemela anayeishi nchini Uingereza alibomoa nyumba hiyo aliyokuwa anaishi Diana bila ya kuvunja mkataba wa upangaji wala kumpa taarifa ya kufanya tukio hilo.
Diana akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Hemed wa Mahakama hiyo ya Nyumba ya Kinondoni alidai kuwa, Lubomola alibomoa alikwenda nyumbani kwake na kutoa milango na madirisha wakati mvua ilikuwa ikinyesha.
Alidai kuwa wakati Lubomola akifanya uharibifu huo, jirani yake alimpigia simu na kumuuliza uko wapi mbona nyumba yako inabomolewa na kutolewa milango, nyavu na madirisha.
Aliendelea kudai kuwa Lubomola wakati akifanya tukio hilo alikuwa na vijana wahuni wa Sinza ambao waliiba droo zake mbili zilizokuwa na nyaraka zake mbalimbali ikiwamo mikataba ya upangaji aliyoingia na mtuhumiwa huyo.
Aliongeza kwa kudai kuwa baada ya kufika nyumbani kwake na kushuhudia tukio hilo alimuita balozi na baadaye alikwenda katika kituo cha polisi cha Urafiki kuripoti na kupewa RB namba UPR/3876/2012 na UPR/4585/2012 kwa ajili ya kumkamata.
Diana alidai kuwa alipomuuliza Lubomola kwanini alifanya hivyo kwa kinywa chake alimwambia kuwa “amepata mtu wa hela ndefu”.
0 comments:
Post a Comment