BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAFISADI WA VIWANJA CCM KUNYANG'ANYWA.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha mapainduzi(CCM),Majura Bulembo akionyesha moja za mikataba kati ya jumuiya hiyo na Mmiliki wa Shule za Green Acres iliyokiukwa jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Katibu wa jumuiya hiyo, Khamis Dadi. Picha na Fidelis Felix.

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeanza kukunjua makucha na kuwatangazia mafisadi waliovamia viwanja vyake kuvisalimisha mara moja vinginevyo watanyang'anywa kwa nguvu.
Uamuzi wa jumuiya hiyo umekuja ikiwa ni takriban mwezi mmoja baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuueleza mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma kwamba mali za jumuiya hiyo zikiwemo shule zimeuzwa na kumilikishwa watu binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema kuwa, kamwe mali za umoja huo haziwezi kuendelea kuwa `shamba la bibi.’

Alisema asilimia 85 za rasilimali za jumuiya  hiyo zilizovamiwa na watu mbalimbali ziko katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Uvamizi mkubwa wa mali za Jumuiya ya Wazazi umefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam. Kazi yetu ya kwanza sasa ni kuhakikisha kuwa, mali hizo zinarudishwa katika jumuiya vikiwamo viwanja,” alisema Bulembo ambaye alichaguliwa kashika nafasi hiyo mwezi uliopita.

Bulembo alitoa mfano kuwa, kiwanja cha jumuiya hiyo kilichopo Sinza/Shekilango, wilayani Kinondoni chenye ekari sita kimevamiwa na kujengwa nyumba 104 za watu mbalimbali zikiwemo sehemu za biashara.
“Tunaomba wavamizi hao wajitathimini wenyewe na kuchukua hatua za kurejesha viwanja hivyo kabla hatujawachukulia hatua na kuwasababishia usumbufu,” alisema Bulembo.

Aliweka bayana kuwa, wavamizi hao hawana hati halali za kujenga katika maeneo hayo labda kama ni za kughushi.
Alizitaja baadhi ya rasilimali za jumuiya hiyo zilizo mikononi mwa watu kuwa ni shule za sekondari 71 na viwanja 121 ambavyo viko katika mikoa mbalimbali nchini.

Licha ya Mwenyekiti huyo kukosa takwimu kamili za viwanja na shule zilizopo katika migogoro, alisema bado wanaendelea kufanya tathimini ili kubaini mali zaidi za jumuiya hiyo ambazo zimevamiwa.
Mwenyekiti huyo alisema jumuiya hiyo haitauza shule zake, bali itazibadilisha matumizi zile ambazo hazifanyi vizuri kuwa vyuo vya ufundi.

“Kila kanda itakuwa na vyuo vya ufundi vinavyofanana na Veta lakini vyuo vya jumuiya vitakuwa vitachukua wanafunzi waliomaliza darasa la saba tofauti na Veta ambao huchukua wanafunzi waliomaliza kidato cha nne,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa, lengo la mpango huo ni kuliwezesha kundi la vijana wanaomaliza darasa la saba kujiunga na vyuo hivyo ili kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri.

“Hivi sasa vijana wakimaliza darasa la saba wanakosa shughuli za kufanya, hivyo tunataka wapate mafunzo ya ufundi yatakayowawezesha kupata ajira, au kujiajiri wenyewe,” alisema Bulembo.
Kada wa CCM naye matatani
Mwenyekiti huyo alisema Jumuiya yake ina mpango wa kuichukua Shule ya Sekondari ya Kaole, iliyopo Wilayani Bagamoyo kwa madai kuwa, mmiliki wa shule hiyo ambaye ni kada na kiongozi wa CCM, Julian Bujugo alikiuka mkataba wa kuiendesha shule  na kubadilisha matumizi na kuifanya kuwa chuo.

Alisema kwenye mkataba huo alitakiwa kuiendesha shule hiyo kama ilivyo bila kuibomoa wala kujenga upya ili mandhari yake ibakie kuwa ileile ya zamani.

Bulembo alisema lengo la kufanya hivyo ni kuibakisha sura ya  kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji na kwamba uwepo wake ulikuwa sehemu ya historia.
“Tulitaka matumizi yasibadilike kwa sababu lile ni eneo la historia kwa Tanzania na Msumbiji kwa kuwa, pale kuna makaburi ya wapigania uhuru wa Msumbiji ambao  mara nyingi hutembelea mahali pale, lakini kuna mabadiliko yamefanyika,”  Bulembo alisema na kuongeza:
"Bujugo ni kada mwenzetu na kiongozi wa CCM, tumemwita aje ofisini tunadhani tutafikia mwafaka wa hili.”
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi baadaye jana, Bujugo alisema; "Ni kweli shule ni ya Wazazi, lakini wenyewe iliwashinda na ndiyo maana tukaingia mkataba wa mimi kuiendeleza.

"Pia kuna mkataba wa kufanya maboresho na kuendeleza shule kuwa Chuo cha Kilimo. Nawashangaa kutoa kauli hizo, kwani mimi nina nyaraka zote za kuniruhusu kuendeleza chuo."

Pamoja na ufafanuzi wake, Bujugo alidai kwamba hakuwa na taarifa za kuitwa Ofisi ya Wazazi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: