Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari Bandarini jijini Dar es salaam jana jioni wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa malori 26 kinyemela bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.
Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini hapo.
Dk. Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia) anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo akijitetea mbele ya Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilojana jioni. Kushoto ni Mkuu wa Polisi Bandarini Afande FM MisilimuOfisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe
Mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kawaida katika idara yake.
0 comments:
Post a Comment