GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4 Ajali mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
0 comments:
Post a Comment