BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

STARS NA AMAVUBI MECHI YA KISASI LEO DIMBA LA NAMBOLE NCHINI UGANDA.


Beki wa Kilimanjaro Stars, Erasto Nyoni (kushoto) akiwania mpira na beki wa Sudan, Faris Abdallah wakati wa mchezo wa Kombe la Chalenji uliochezwa jana kwenyeUwanja wa Nambolee,Kampala. Tanzania ilishinda 2-0.  


TIMU za Tanzania, Kilimanjaro Stars (Bara) na Zanzibar Heroes ya visiwani Zanzibar, leo zitakuwa na mtihani mzito wakati zitakaposhuka dimbani kwa nyakati tofauti kuzikabili Rwanda na Burundi katika mapambano ya robo fainali ya kwanza ya Michuano ya Chalenji inayoendelea kutimka vumbi jijini hapa.
Stars itakuwa ya kwanza kuingia uwanjani ikipambana dhidi ya Rwanda katika pambano litakalopigwa kwenye dimba la Kagogo saa 8 mchana, wakati ndugu zao wa Heroes watasubiri mpaka saa 10 jioni kuwavaa Burundi kwenye Uwanja huohuo.
Katika pambano hilo, Stars itaingia uwanjani kwa lengo moja la kutaka kulipa kiasi baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka Amavubi kwenye Michuano ya Chalenji iliyofanyika mwaka jana jijini Dar es Salaam kutokana na timu hizo kukutana katika hatua ya makundi.

Kwa upande mwingine, Amavubi bado ina hasira za kuzabuliwa bao 1-0 na Stars baada ya timu hizo kukutana katika mechi ya hatua ya nusu fainali ya Chalenji iliyofanyika Dar es Salaam.
Timu zote mbili zitaingia uwanjani katika hali ya kujiamini baada ya kushinda mechi zao za mwisho za kukamilisha hatua ya makundi. Stars iliitungua Somalia mabao 7-0, wakati Amavubi iliichapa Eritrea mabao 2-0.
Winga wa Stars Mrisho Ngasa anayeongoza katika orodha ya wafungaji baada ya kufunga mara tano kwenye mchezo mmoja, anatarajia kuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Amavubi.

Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema anatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka Rwanda kwenye mchezo huo, lakini akasema atatumaini kikosi chake kilichosheheni vijana wengi.
Kwa upande wake, kocha wa Amavubi, Milutin’Micho’Sredojovic amesema anaiheshimu Stars kama moja ya timu imara kwenye michuano, ingawa kikosi chake pia kitatumia ubora kilionao kuhakikisha kinawanyamazisha Watanzania.
Naye kocha wa Heroes, Salum Bausi amesema haiofii Burundi licha ya kwamba imetinga katika hatua ya robo fainali pasipo kupoteza mchezo hata mmoja.

Pamoja na hayo, Heroes italazimika kucheza kwa tahadhari ili kukwepa moto wa Burundi, ambaye kocha wake amesema lengo lake ni kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa staili ya ushindi wa asilimia 100.
Robo fainali ya pili itapigwa kesho kwenye dimba la Namboole, ambapo wenyeji Uganda watakwaana na Ethiopia saa 1 usiku, wakati Kenya itaumana na Malawi.

Kipa wa Heroes Mwadin Ali amesema hawaiogopi Burundi, na kwamba wapo tayari kukabiliana nayo na kufuzu hatua ya nusu fainali.
“Burundi tunaiheshimu kama timu nyingine zote zilizoingia hatua ya robo fainali, hivyo hakuna sababu ya kuwaogopa,” alisema Mwadini.
Akizungumzia kipigo cha mabao 2-0 walichokipata kutoka kwa Malawi katika mechi ya kukamilisha hatua ya makundi, alisema kilitokana na wao kuamua kucheza kwa tahadhari ya kuepuka kuumia hasa baada ya kujua tayari walishafuzu.

Kwa upande wake, nahodha wa Stars, Juma Kaseja amesema mchezo huo ni wa kucheza kwa kujituma kwa vile Rwanda ni miongoni mwa timu nzuri kwenyema shindano.
“Tumejipanga vizuri, kila mchezaji anafahamu kwamba anakwenda kucheza na timu ya aina gani. Dhamira yetu ni kupata ushindi, akili yetu iko kwenye ushindi,” alisema Kaseja.

Kaseja alisema kuwa, kikosi chao kitacheza kufa au kupona ili kuhakikisha kinaiondoa Amavubi mashindanoni na wao kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali.
“Hatufurahii matokeo mazuri dhidi ya Sudan, kwetu muhimu ni kwamba tumefika hatua ya robo fainali na sasa tunaangalia kucheza nusu fainali,” alisema Kaseja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: