BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WFP: NCHINI NNE ZAHITAJI MSAADA WA CHAKULA KUSINI MWA AFRIKA.

 
SHIRIKA la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa zaidi ya watu milioni 3.5 walio nchini Malawi, Zimbabwe na Lesotho wanahitaji msaada wa chakula kwa muda wa miezi minne ijayo wanapongojea msimu wa mavuno.

Kiasi kidogo cha mvua maeneo ya kusini mwa Afrika kimesabisha kushuhudiwa uhaba wa chakula kwenye nchi hizo tatu huku mahitaji yakitarajiwa kuongezeka katika ya msimu wa upanzi ambao ni mwezi Oktoba na Novemba na wa kuvuna mwaka ujao.

Bei ya mahindi imeongezeka kwa asilimia 60 kwenye masoko nchini Lesotho tangu mwanzo wa mwaka.

Nchini Malawi nako bei ya mahindi imepanda kwa silimia 80 tangu wakati kama huu mwaka uliopita. 

WFP inasema kuwa kupitia usaidizi wa serikali , wahisani na mashirika mengine inakusanya misaada kuwasaidia walio na mahitaji zaidi. 

Elizabeth Byrs, ni msemaji wa WFP.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: