SHIRIKA la kimataifa la Uhamiaji IOM limesema wahamiaji wanaathirika
zaidi na virusi vya ukimwi na Ukimwi hususan katika nchi zenye vipato
vya juu.
IOM inasema kuwa ripoti ya mwaka huu ya UNAIDS inaonyesha kuwa kwa
mara kwanza katika historia ya Ukimwi, maambukizi mapya ya ugonjwa huo
katika nchi zilizokuwa na mzigo mkubwa wa maambukizi hayo yanapungua,
lakini bado kuna changamoto.
Ripoti hiyo inatoa mfano wa nchi zenye vipato vya juu kama zile za
Amerika Kaskazini na Ulaya ambako inasema idadi ya watu wanaoishi na
virusi vya Ukimwi imeongezeka katika kipindi cha miaka Kumi iliyopita.
Imesema wahamiaji na watu wanaohamahama wako hatarini zaidi
kuambukizwa virusi hivyo kwa sababu mipango mingi ya afya huwaengua mara
kwa mara na hata hawawezi kupata huduma za afya.
Jumbe Omari Jumbe ni
msemaji wa IOM
0 comments:
Post a Comment