Kwa ufupi:
Katika pambano la kwanza lililofanyika jijini Dar es
Salaam wiki moja iliyopita, Simba ililala kwa bao 1-0, hivyo inahitaji
ushindi wa zaidi ya mabao mawili katika mchezo wa marudiano ili iweze
kusonga mbele.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tzKOCHA, MILOVAN CIRKOVIC.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tzKOCHA, MILOVAN CIRKOVIC.
ALIYEKUWA kocha wa Simba, Milovan Cirkovic amesema Simba haina
uwezo wa kuifunga Libolo katika pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa
Afrika litakalopigwa Machi 2 jijini Luanda, Angola.
Katika pambano la kwanza lililofanyika jijini Dar
es Salaam wiki moja iliyopita, Simba ililala kwa bao 1-0, hivyo
inahitaji ushindi wa zaidi ya mabao mawili katika mchezo wa marudiano
ili iweze kusonga mbele.
Akizungumza na gazeti hiliMwananchi jijini Dar es
Salaam, Cirkovic alisema kuwa, aina ya soka linalochezwa na Simba hivi
sasa siyo la malengo wala ushindani na zaidi halitaweza kuisaidia timu
hiyo kuifunga Libolo katika pambano la marudiano.
“Simba hii siyo ile niliyoiacha wakati ule,
haichezi soka la ushindani kabisa, nadhani kuna tatizo ambalo linatakiwa
kufanyiwa kazi,”alisema Cirkovic.
Alisema,”Kkwa aina ya soka nililolishuhudia,
hakika hakuna uwezekano wa kuifunga Libolo katika pambano la marudiano,
ukiwaangalia wachezaji utawaona wanacheza kama vile kwa ajili ya
kujifurahisha na siyo kusaka ushindi, yaani kifupi ni kwamba hawana
morali.”
Cirkovic alisema kuwa kuna haja ya uongozi wa
Simba kukaa na wachezaji wao ili waweze kufahamu kile kinachowasibu na
kukipatia ufumbuzi kabla mambo hayajaharibika zaidi.
“Ukiangalia wachezaji ni walewale niliowaacha,
kama kuna wapya basi ni wachache tu ambao hata hivyo siwaoni wakipata
nafasi, jambo la msingi wakae na wachezaji wawaambie wana matatizo gani
ili wayatatue kabla mambo hayajaharibika zaidi,”alisema Cirkovic.
SIMBA WAKUTANA
SIMBA WAKUTANA
Baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa
Mtibwa Sugar, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage jana jioni aliitisha
kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na kuahidi kufanya uamuzi
mgumu.
Rage alisema ameitisha kikao cha utendaji ili kujadili mwenendo wa timu yao na kuahidi kutoka na uamuzi mzito.
‘’Anayetakiwa kuulizwa kwa nini timu haifanyi
vizuri ni kocha Patrick Liewig na benchi la ufundi siyo viongozi, mimi
nimeishakaa na benchi la ufundi nikaongea nao na wakatuambia tatizo ni
nini, hivyo wanachama wasubiri uamuzi utakaofanywa na Kamati ya
utendaji,’’ alisema Rage.
Pia, Rage alisisitiza hawezi kujiuzulu kama watu
wanavyodai kwa kuwa kosa la timu kufanya vibaya siyo lake bali la benchi
la ufundi, anachotakiwa kuulizwa yeye ni kama timu haijalipwa
mishahara, haina sehemu ya kulala haijapewa fedha zao za usajili na siyo
timu kufaya vibaya uwanjani.
0 comments:
Post a Comment