YA TANZANIA.
KUTOKANA na wanasiasa na wadau mbalimbali wa elimu kumsakama Waziri Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii inatokana na Viongozi wetu wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile wanachokisema.
Tanzania tuna Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena wengine wa siku nyingi lakini hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu ya Tanzania zaidi wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya kutoa ufumbuzi wa namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.
Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni malumbano yasiyokuwa na tija.

Hata tume inayotazamiwa kuundwa na waziri mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi kabla hata tume haijaanza kazi.
Tunajua Maprofesa na Madokta (PhD) wana uwezo mzuri wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu hata kutunga Vitabu vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao cha elimu lakini tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake wakati tuna wasomi wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu bali tuwe Taifa la kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.
Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana
kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya siasa.
Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana
kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya siasa.
Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado serikali inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni midogo sana na haiendani kabisa na mazingira wanayoishi.
Mwalimu mwenye degree analipwa takribani 500,000/= na usheee, diploma takribani 300,000/= na ushee na mwenyecheti takribani 200,000/= na ushee unategemea nini hapo ?.
Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli mtu una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf ,
ukatwe CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.

1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame.
Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara ya walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na wanaishi maisha ya kifahari kuliko sisi walimu.
Tulitegemea wabunge wange wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili wafanye kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa.
Mwalimu hata angejituma vipi kama mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana lazima awaze kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana hata motisha.
Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.
Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015

0 comments:
Post a Comment