BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BURKINA FC YAMALIZA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA KWA AIBU.


Mshambuliaji wa JKT Mlale ya Songea, Kudra Omari kulia akimtoka mlinzi wa Burkina FC Joseph Nditi kushoto wakati wa mchezo wa kukamilisha ratiba wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Burkina FC kufungwa bao 4-2 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.


Na Juma Mtanda.
TIMU ya soka ya Burkina FC ya Morogoro imemaliza ligi daraja la kwanza kwa aibu baada ya kupokea kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa JKT Mlale katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Katika mchezo huo Burkina FC ndiyo walianza kufumania nyavu kwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji, Joseph Justine aliyefunga katika dakika ya 19 kwa kichwa baada krosi ya mlinzi Mwatindi Benard.

JKT Mlake kutoka mkoani Songea ilisawazisha bao hilo katika dakika 40 kupitia kwa kiungo mshambulia Saidi Ally kumpiga chenga mlinzi wa Burkina na kufumua shuti kali eneo la hatari na mpira kujaa wavuni kabla ya mshambuliaji mongwe Kudra Omari kuandika bao la pili dakika ya 42 na kwenda mapumziko wakiwa na bao 2-1.

Kipindi cha pili JKT Mlale waliendeleza kasi na kuwapeleka puta ngome ya ulinzi ya Burkina FC na katika dakika ya 50 Ally Saidi aliandikia timu yake bao la tatu likiwa bao la pili kufunga baada ya kumpiga chenga mlinda mlango wa Burkina FC, Mohamed Athman na kujaza mpira kimiani kabla ya Francisco Bruno kukamilisha kalamu ya mabao dakika ya 76 kwa shuti la umbali wa mita 20.

Burkina FC walipata bao la pili kupitia kwa Hmais Rashid aliyefunga kwa mkwaju wa penalti 87 baada ya kuangushwa kwa mshambuliaji wao na mwamuzi, Steven Makuka kutoka Iringa kutoa adhabu hiyo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Burkika FC kufungwa bao 4-2 na JKT Mlale.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: