Na Haruni Sanchawa, Pwani.
DUNIA ni
mbaya, kwani haiwezi kuwa nzuri kama mauaji ya kinyama yataendelea
kushamiri, binadamu wakichinjana utadhani hakuna dola wala Mungu.
Fatma
Shaban, 24, mkazi wa Mpiji Mgohe, Kinondoni, Dar es Salaam, ameuawa kwa
kukatwakatwa mapanga, viungo vyake kugawanywa kisha akatolewa utumbo.
Anayetuhumiwa
kumfanyia unyama huo ni mumewe, Peter Ndala, 23, ambaye kabla ya
migogoro, walishirikiana vizuri na kuchangia mambo mengi ya kimapenzi.
Unyama huo, ulitendeka Machi 7, mwaka huu, eneo la Kidimu ambalo ni mpaka unaoigawa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Habari zilizothibitishwa ni kuwa Fatma na Ndala, walikuwa wakiishi pamoja kama mke na mume, wakapata mtoto mmoja.
Uwazi
halina uthibitisho kama wawili hao walifunga ndoa, ila limeelezwa kuwa
Fatma na Ndala walitofautiana na kuanza kuishi kila mtu kivyake.
UKATILI ULIANZA KWA WEMA
Habari
kutoka kwa vyanzo vyetu zinasema kuwa siku ya tukio, Ndala alimtembelea
Fatma kwenye sehemu yake ya biashara, alikokuwa anajishughulisha na kazi
ya mama lishe.
“Alipofika
pale alipewa chakula na huyo mzazi mwenzie kisha akala. Ilipofika saa 2
usiku, Fatma alifunga biashara yake na kuanza safari yake ya kwenda
nyumbani kwao ambako alikuwa anaishi kwa dada yake.
“Waliongozana
pamoja, lakini wakati wanaelekea nyumbani mazungumzo yao hayakuwa
mazuri, hivyo yule mwanaume akachukizwa na kuamua kumfanyia ukatili huo
mzazi mwenzake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza.
“Ndala
alimkatakata Fatma, mikononi alimkata vipande viwili, akamchoma tumboni,
akamtoa utumbo, baada ya hapo akatokomea kusikojulikana.
“Fatma alipiga kelele, majirani walikimbia kwenda kumuokoa na wakakuta muuaji ametoweka.”
Chanzo
chetu kiliongeza, Fatma kabla ya kufariki dunia, aliwaambia watu
waliofika kumwokoa kwamba aliyemtenda unyama huo ni mzazi mwenzake kisha
akamtambulisha kwa majina matatu ya Peter Ndala Kasheba.
RPC KAZINI
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulricha Matei alisema: “Ni kweli tukio hilo
lilitokea na tunamsaka muuaji kwa kushirikiana na polisi wa Kinondoni.”
NA GLOBAL PUBLISHER
0 comments:
Post a Comment