Kwa ufupi
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi
Jumamosi Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa
alithibitisha kwamba jeshi lake limekuwa likishirikiana na FBI katika
upelelezi huo na kwamba idadi ya waliokamatwa imeongezeka.
UJIO wa Askari wa Shirika la Upelelezi la
Marekani (FBI) nchini na kuanza kufanya kazi, umewezesha kuanza kunaswa
kwa baadhi ya watu, wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Padre Evarist Mushi
(55) wa Kanisa Katoliki Unguja, visiwani Zanzibar.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumamosi Dar es Salaam jana,
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa alithibitisha kwamba jeshi
lake limekuwa likishirikiana na FBI katika upelelezi huo na kwamba idadi
ya waliokamatwa imeongezeka.
“Ni kweli tumekuwa tukishirikiana na
FBI katika upelelezi ili kuhakikisha kuwa, wahusika wa tukio la kuuawa
kwa Padri Mushi wanakamatwa. Hii itasaidia kupunguza vitendo
vinavyohusishwa na matukio ya kigaidi yakiwamo mauaji,”alisema Kamishna
Musa.
Alisema kuwa hilo linafanyika ili kuhakikisha kuwa, zoezi la
kuwakamata wahusika wa uhalifu huo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa,
jambo alilosema linaweza kupunguza matukio ya mauaji.
Alibainisha
kwamba hadi sasa kuna ongezeko la idadi ya watu waliokamatwa na kwamba
watu hao wanaendelea kuhojiwa, huku wengine wakishikiliwa kwa sababu
maalumu.
Kamishna Musa alifafanua kuwa kutokana na zoezi hilo
watu watakaobainika kuhusika na mauaji hayo watafikishwa kwenye vyombo
vya sheria ili wachukuliwe hatua zaidi.
Padri Evaristus Mushi
aliuawa Februari 17, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana
waliokuwa katika pikipiki aina ya Vespa, wakati akienda kuongoza misa
katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.
Juzi,
Kamishna Musa aliliambia Gazeti hili kwa njia ya simu kwamba wapelelezi
wa kigeni wamewasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua
kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi.
Alisema kuwa wapelelezi
hao tayari wameanza kazi hiyo kushirikiana na wenzao wa Tanzania
kuwasaka wauaji wa padri huyo aliyepigwa risasi Februari 17, mwaka huu.
“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” alisema Kamishna Mussa bila ya kutaja wanatoka nchi gani. Pia Kamishna Mussa hakutaka kueleza ni lini wapelelezi hao walifika Zanzibar na idadi yao kwa maelezo kwamba hizo ni siri za polisi na kwamba zikivuja, zitaingilia uchunguzi wanaoufanya. Hata hivyo, vyanzo vya ndani ya Serikali, vililithibitishia Mwananchi kuwa FBI walikuwa wameanza kuwasaka wauaji wa Padri Mushi. Kutua kwa wapelelezi hao wa Marekani kunafuatia kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi, kuwa amewaagiza polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya ndani na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo. Awali, akitoa tamko la Serikali na kueleza kuwa Rais Kikwete ameidhinisha Serikali kugharamia wapelelezi kutoka nje, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alihusisha tukio hilo na vitendo vya ugaidi. Ujio huo wa FBI pia unaweza kuhusishwa moja kwa moja na dhamira iliyoonyeshwa mapema na Serikali ya Marekani kuwa ipo tayari kusaidia upelelezi wa mauaji hayo. Dhamira hiyo ilibainishwa katika salamu za rambirambi za kifo hicho zilizotolewa na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt. Vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya Serikali vimeeleza kuwa kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo, maofisa wa FBI walifanya mazungumzo na Waziri Nchimbi na viongozi wengine wa Serikali kwa ajili ya kuangalia namna watakavyofanya shughuli hiyo.

0 comments:
Post a Comment