PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Alfonce Twimann’ye
mwishoni mwa wiki alilazimika kujificha katika nyumba ya watu baada ya
kukimbizwa na watu wasiojulikana eneo la Nyakato mkoani Mwanza.
Habari za kuaminika na zilizothibitishwa na padri huyo maaarufu kwa
mahubiri mkoani hapa, zimesema kuwa watu wawili waliokuwa katika
pikipiki, walimwandama wakati akielekea Kitongoji cha Mahina kutoa
huduma za kiroho kwa mmoja wa waamini wa Kanisa Katoliki.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi kwa njia ya simu, Padri Alfonce alisema akiwa katika kituo kimoja cha mafuta eneo la Nyakato wiki iliyopita, alishangaa kuona kwa mbali kikundi cha watu kikimtazama na baadhi yao wakioneshana vidole kumwelekea alipokuwa ameegesha gari.
Padri huyo aliongeza kuwa, wakati anaondoka baada ya kuweka mafuta katika gari, watu wawili waliokuwa katika pikipiki walimfuata, kwa mwendo wa kasi jambo lililompa wasiwasi.
“Nilipata hofu na kuongeza mwendo huku nikijitahidi kuzuia wasinipite, na kubadili mwelekeo na kuingia mtaa mwingine.
“Watu hao nao walikata kona na kunifuata, wakijaribu kunisogelea zaidi, lakini walishindwa kunipita kwa sababu njia ilikuwa na msongamano kidogo wa watu,” alisema.
Padri huyo alisema alibadili tena mwelekeo na kuingia mtaa mwingine, lakini bado alizidi kuandamwa na alipoona hakuna usalama, alilazimika kuegesha gari karibu na nyumba moja na kukimbilia ndani.
“Najua hata wenyeji wangu walinishangaa, na sikutaka kuwapa hofu, bali nilitulia na kuanzisha mazungumzo mengine, lakini akili na masikio yangu yakiwa nje,” alisema.
Aliongeza kuwa watu hao walisimama mbele kidogo na alipoegesha gari lake, na baada ya kusubiri kwa muda mrefu waliondoka, na alipohakikisha kuna usalama aliondoka kurejea nyumbani.
Alisema kabla ya tukio hilo, Jumatatu wiki iliyopita, majira ya saa moja usiku watu watatu wenye asili ya Kiarabu wakiwa na gari, walifika katika makazi ya mapadri hao huko Bugando na kutaka kuonana na mmoja wao.
“Walimlazimisha mlinzi awaoneshe kwanza padri ambaye hawakuweza kumtaja jina, lakini walipobanwa, wakasema wanamtaka yeyote aliyepo.
“Mlinzi alipowauliza shida yao na kwa nini waje usiku, watu hao walikuja juu wakitaka waruhusiwe kumwona padri, na kwamba sio kazi ya mlinzi kuwahoji,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, alidai kutojua tukio hilo.
“Sijapata taarifa hiyo. Lakini nataka kusema wazi kuwa watu wasiogope kwa sababu kuna ulinzi wa kutosha, na kama mtu anahisi kuwepo kwa hatari atoe taarifa mara moja,” alisema.
Hata hivyo, alionya dhidi ya watu wanaojaribu kuleta hofu miongoni mwa wananchi, na kwamba jeshi hilo litamchukulia hatua yeyote anayesambaza vitisho dhidi ya viongozi na waumini wa dini.
JK: Tutapambana na wachochezi
Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete amesema serikali itawachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaokejeli na kudharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine.
Katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi aliyoitoa jana, Rais Kikwete alisema kumekuwepo na matumizi mabaya ya redio, simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini mbili kubwa hapa nchini.
Alisema kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama vilivyotokea huko Geita na Zanzibar.
Rais Kikwete alisema kutokana na hali hiyo, amelitaka Jeshi la Polisi na mamlaka zingine kuwachukulia hatua stahiki wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini ipasavyo, ambao wanaleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia.
“Nimewakumbusha polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo… wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika na kuwataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao “ajizi nyumba ya njaa”.
Lowassa ataka wavurugaji wasionewe aibu
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameitaka serikali kutumia nguvu zake zote kudhibiti chokochoko na viashiria vyote vinavyoweza kuvuruga amani ya nchi.
Alisema ni lazima serikali na viongozi wa kada zote wasimame imara kutetea na kulinda amani iliyodumu tangu uhuru, kiasi cha kuyafanya mataifa ya nje yamezee mate utulivu uliopo nchini.
Lowassa aliyasema hayo jana wakati wa misa maalumu ya kuwaombea wanawake duniani, iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa mfuko wa akina mama wajasiriamali (VIKOBA), wa makanisa ya Kikristo (CCT), Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza, uliofanyika kwenye Kanisa la Anglikana Nyamanoro, ambapo jumla ya sh milioni 40 zilichangwa.
"Tuisafishe nyumba yetu ili Tanzania iwe ya amani. Maana nchi yetu kwa sasa inaonekana kuwa na migogoro ya amani. Watanzania tusichoke na amani, wasichezee mboni ya jicho la amani ya nchi yetu.
"Nahubiri amani, nahubiri amani...usiruhusu mtu aje afanyie mazoezi yake kwenye mboni yako ya jicho. Tusiruhusu hata kidogo mtu au watu wachezee hii mboni, maana ikishatoka haitarudi tena," alisema Lowassa.
Hata hivyo, aliwapongeza na kuwaomba viongozi wa dini zote wakiwemo maaskofu, wachungaji na masheikh pamoja na Rais Kikwete kuendelea na juhudi zao za kukemea vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
"Nawapongezeni sana viongozi wote wa dini pamoja na rais wa nchi, wadau wa amani na wananchi wote kwa kutaka nchi yetu iwe na amani kama iliyokuwepo tangu uhuru.
"Waganda na wagombea urais Kenya wanataka wachaguliwe ili wadumishe amani kama ilivyo Tanzania. Tuwakataeni na kazi ya kulinda amani siyo ya rais wala maaskofu pekee, bali yetu sote," alisisitiza Lowassa.
Kumekuwa na taarifa nyingi zinazotumwa kwa njia ya mtandao zikionesha kuwepo kwa kikundi cha watu wanaotaka kuanzisha vurugu za kidini zinazoweza kuambatana na madhara kwa wafuasi wa dini nyingine.
Sheikh Khalifa atoboa siri
Jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi maarufu wa Kiislamu, Sheikh Khalifa Khamis amefichua siri ya kuwepo kwa kikundi cha Kiislamu kinachoendesha vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kutoa mafunzo ya kareti misikitini.
Katika taarifa yake kuhusiana na matukio ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Sheikh Khalifa pamoja na kulaani vikali mauaji hayo, alidai kuwa kikundi hicho (jina limehifadhiwa) kimekuwa kikiendesha operesheni za kuteka misikiti ambayo inaendeshwa na bodi za wadhamini waliosajiliwa kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Wanavamia na wanatangaza hadi kwenye magazeti kuteka misikiti ambayo wanaigeuza kuwa vituo vya kujifunzia kareti na kufanyia mikutano na hotuba za kuwahamasisha Waislamu kufanya vurugu, na wadhamini halali wa misikiti hiyo wanapolalamika wanabezwa na vyombo vya dola.
“Wamekuwa na jeuri ya kupinga hata amri zilizotolewa na mahakama huku vyombo vya dola vikishuhudia, hatua ambayo imekifanya kikundi hiki kujidhani kuwa kiko juu ya sheria,” alisema Sheikh Khalifa ambaye amekwenda mbali na kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kujiepusha nacho.

TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment