Kwa ufupi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeiamuru
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasilishe majalada ya kesi ya ugaidi
inayomuhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare na mwenzake katika kesi hiyo, Ludovick Joseph.
http://www.mwananchi.co.tz![http://www.mtanzania.co.tz/images/stories/kitaifa/lwakatare.jpg](http://www.mtanzania.co.tz/images/stories/kitaifa/lwakatare.jpg)
Dar es Salaam. ![http://www.mtanzania.co.tz/images/stories/kitaifa/lwakatare.jpg](http://www.mtanzania.co.tz/images/stories/kitaifa/lwakatare.jpg)
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasilishe majalada ya kesi ya ugaidi inayomuhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake katika kesi hiyo, Ludovick Joseph.
Hati ya kuitisha majalada hayo ilitolewa jana
alasiri na Msajili wa Mahakama Kuu, baada ya mawakili wanaomtetea
Lwakatare kuwasilisha maombi ya marejeo ya mwenendo wa kesi hiyo,
iliyofunguliwa katika Mahakama ya Kisutu.
Maombi hayo ya marejeo yaliwasilishwa mahakamani
hapo jana chini ya hati ya dharura yakiambatanishwa na hati kiapo ya
mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, Peter Kibatala. Wengine ni
Mabere Marando, Profesa Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na Tundu
Lissu.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata kisha baadaye
kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare zilisema kuwa
jana Msajili wa Mahakama Kuu alisaini na kutoa hati hiyo kwenda Mahakama
ya Kisutu.
Mapema jana mawakili wanaomtetea Lwakatare waliwasilisha maombi hayo ambayo yalipokewa na kupewa usajili wa namba 14 ya 2013.
Mawakili hao wanaiomba Mahakama Kuu, iitishe
majalada yote mawili ya kesi hiyo, jalada namba 37 ya mwaka 2013 na
namba 6 ya mwaka 2013 kwa ajili ya uchunguzi ili iweze kujiridhisha
usahihi na uhalali wa mwenendo wake.
Pia wanaiomba Mahakama Kuu ifanye marejeo na/au
kutengeua hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyowafutia mashtaka
watoa maombi (Nolle Prosequi) kabla ya kuwakamata na kuwafungulia tena
mashtaka hayohayo.
Maombi yao mengine ni kutaka Mahakama ya Kisutu
iamriwe kutoa uamuzi wa maombi ya dhamana, uliokuwa umepangwa kutolewa
na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emillius Mchauru, Machi 20, 2013, katika
kesi namba 37.
Mawakili hao wanadai kuwa uamuzi huo ambao ulihusu
dhamana ya watuhumiwa, ulitenguliwa na hati ya DPP ya kuwafutia
mashtaka washtakiwa hao, isivyo halali.
Maombi mengine ni kurejea na/ au kutengua mwenendo
wa kesi namba 6 iliyofunguliwa baada ya hati ya kuwafutia mashtaka
watoa maombi hao na badala yake iendelee kesi namba 37.
Wanaiomba pia Mahakama Kuu iamue kwamba utaratibu
uliotumiwa na wajibu maombi (Jamhuri) kutoa hati ya kuwafutia mashtaka
watoa maombi katika kesi namba 37 ilikuwa kinyume cha sheria na/ au
haukuwa sahihi.
Wanadai kuwa utaratibu huo ulisababisha matumizi
mabaya ya taratibu za kimahakama na matumizi mabaya ya mamlaka ya
kiuendeshaji mashtaka na kushusha hadhi na uhuru wa mahakama.
0 comments:
Post a Comment