Abdiaziz Abdinuur Ibrahim.
MAHAKAMA makuu ya mjini Mogadishu Somalia yamemwaachilia huru mwandishi
wa habari ambaye alifungwa kwa sababu ya kumhoji mwanamke aliyesema
amebakwa.
Katika kesi iliyolalamikiwa kimataifa, mwandishi huyo, Abdilaziz
Abdinuur, awali alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja kwa kumhoji
mwanamke ambaye alisema alibakwa na wanajeshi wa serikali.
Mwanamke huyo piya alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja lakini kesi yake ilifutwa kwenye rufaa awali mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment