Kwa ufupi
Papa Francis ameadhimisha misa yake ya kwanza tangu
alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, huku
akitoa hotuba ya dakika tano mbele ya waumini wa Parokia ya Mtakatifu
Anna.
Vatican City.
PAPA Francis ameadhimisha misa yake ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, huku akitoa hotuba ya dakika tano mbele ya waumini wa Parokia ya Mtakatifu Anna.
Papa Francis 1 (kulia) akiwa na mtangulizi wake Papa mstaafu Benendict XVI.
PAPA Francis ameadhimisha misa yake ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, huku akitoa hotuba ya dakika tano mbele ya waumini wa Parokia ya Mtakatifu Anna.
Jana, katika mahubiri yake mafupi, Papa Francis
alishangaza wengi kwa kueleza kuwa binadamu hawana budi kusameheana,
kama ambavyo Mungu amekuwa mwenye huruma kwa wanadamu.
Awali, Papa alijitokeza hadharani katika lango kuu
la kuingilia kanisa hilo la parokia akiwa amevaa kanzu nyeupe, viatu
vyeusi, kuwapungia mkono watu wote, kisha kupeana nao mikono.
Kisha, alibusu, kuwashika mabegani watoto na kueleza kuwa jukumu la binadamu ni kupendana.
“Ningependa sisi sote tuwe na ujasiri wa kutembea katika uwepo wa Mungu,” alisema Papa Francis kwa Kilatini.
Mapema, Papa alifanya maombi binafsi katika Kanisa
Kuu la Santa Maria Maggiore na baadaye alikutana na watoto na wasafiri
waliokwenda kumsalimia.
Papa, pia ameanza kazi ya uteuzi wa maofisa wa juu wa Vatican, ingawa orodha hiyo haijakamilika wala kuwekwa wazi.
Jumatano usiku muda mfupi baada ya kuchaguliwa
kwake, aliusalimia umati wa watu waliofurika katika Uwanja wa Mtakatifu
Petro akitoa wito wa unyenyekevu na kuwaomba waumini wamwombee baraka
kabla yeye hajawabariki.
Alhamisi, Papa Francis alirudi kwenye makazi ya
watumishi yaliyopo mjini Rome alipokuwa akiishi mbele ya jengo la
mikutano ulimofanyika uchaguzi uliomweka madarakani.
“Alifungasha mizigo yake na kwenda kulipia chumba alichofikia ili kuwa mfano bora.
“Pia, alivunja utamaduni wa kwenda kuwasubiri
makardinali waliokwenda kumpa pongezi, badala ya kukaa kwenye kiti cha
enzi,” alisema msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi.
Ijumaa alikutana na makardinali 106 wakiwamo wale ambao hawakuingia kwenye mkutano wa uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment