Kwa ufupi:
Hatua hiyo ya ICC imekuja ikiwa ni miezi sita tangu
Serikali ya Tanzania ilipopelekwa katika mahakama hiyo, iliyoko The
Hague, Uholanzi kwa madai ya kukiuka haki za binadamu.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tzRais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka
Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda alipofika
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa
(ICC), Fatou Bensouda, ametua nchini jana na kufanya mazungumzo na Rais
Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.
Hatua hiyo ya ICC imekuja ikiwa ni miezi sita
tangu Serikali ya Tanzania ilipopelekwa katika mahakama hiyo, iliyoko
The Hague, Uholanzi kwa madai ya kukiuka haki za binadamu.
Malalamiko hayo maalumu yalipelekwa ICC na Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Septemba 28 mwaka jana, baada ya
kutokea kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha
Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na watu wengine 23.
Taarifa ya LHRC ilieleza kuwa pamoja na watu hao kuuawa, Serikali ilishindwa kuwachukulia hatua wahusika.
Mbali na kuishtaki Serikali ICC, kituo hicho cha
Sheria na Haki za Binadamu pia kilipeleka mashtaka kwenye Tume ya Afrika
ya Haki za Binadamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk Hellen
Kijo-Bisimba, alisema kuwa walifungua mashtaka hayo ili kuzitaka mamlaka
hizo za kimataifa kufanya uchunguzi na kuichukulia hatua stahiki za
kisheria dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Jana Rais Jakaya Kikwete alikutana na Bensouda na
kufanya mazungumzo na baadaye walipiga picha za pamoja nje ya Viwanja
vya Ikulu, akiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji
Frederick Werema, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi.
Katika maelezo yake Bisimba alisema:
“Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu.”
“Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu.”
“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa
Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile.
Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani,” aliongeza Dk Bisimba.
Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani,” aliongeza Dk Bisimba.
Gazeti hili lilipomtafuta Jaji Werema kuzungumzia
ujio wa Bensouda alisema kuwa Mwendesha Mashtaka huyo alikuwa mgeni wa
Rais Kikwete, hivyo hawezi kueleza kilichozungumzwa.
“Alikuwa mgeni wa Rais, lakini kubwa nililolisikia
ni kwamba alikuja kusalimia kwa sababu tangu alipoteuliwa hakuwahi kuja
Tanzania,” alisema Werema.
Kama ilivyokuwa kwa Werema, naye Feleshi alikwepa
kuzungumzia ujio huo wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, huku akisema
jambo hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Ikulu.
0 comments:
Post a Comment