BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS KENYATTA ATEMBELEA MOMBASA.

Uhuru Kenyatta akipunga mkono mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa Kenya.Rais mteule Uhuru Kenyatta akipunga mkono mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa Kenya.

WANASIASA wakuu nchini Kenya Raila Odinga na mpinzani wake rais mteule Uhuru Kenyatta jumatatu walizulu katika mji wa Mombasa, katika halfa tofauti.
Wiki moja baada ya kutangazwa mshindi, rais meule Uhuru Kenyatta amezulu Mombasa pamoja na familia yake kwa mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Ziara hiyo ni kumbu-kumbu ya jinsi babake hayati Mzee Jomo Kenyatta alivyozuru sehemu hiyo, katika kipindi cha utawala wake akiwa rais wa Kenya kwa miaka 15.

Baadaye alipohutubia mamia ya waumini katika kanisa moja mjini Mombasa, Uhuru Kenyatta ametoa wito wa amani kwa Wakenya, akiwasihi wakatae kugawanywa katika misingi ya kikabila.


Rais huyo mteule anawataka wananchi kuwa na utulivu wakati taifa linaposubiri uamuzi wa mahakama ya juu, kuhusu kesi iliyowasilishwa na wapizani wake, kupinga ushindi wake kama rais wa nne wa Kenya.
Ziara ya Bwana Kenyatta katika eneo hili la Pwani inaonekana kupangwa na muungano wa Jubilee, kwa sababu aliandamana na wafuasi wa muungano huo akiwemo seneta mteule wa County ya Nairobi Mike Mbuvi maarufu kama “Sonko”.

Wakati huo huo Sheikh Juma Ngao –mwenyekiti wa shirika la ushauri wa Kiislamu –KEMNAC, amejitokeza kuitetea tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya –IEBC, kutokana na lawama ilizolimbikiziwa katika uchaguzi huo mkuu, hasa wa urais.


Waziri mkuu Raila Odinga –aliye kinara wa muungano wa CORD naye amezuru Mombasa jumatatu  kukutana na wafuasi wake.

Ameelezea matumaini ya kushinda kesi inayopinga ushindi wa Uhuru Kenyatta, huku akiwasihi wafuasi wake kuwa watulivu hadi pale kesi hiyo itakapo-kamilika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: