TAHADHARI KUHUSU WATU WANAO FANYA UTAPELI MTANDAONI KWA JINA LA TAASISI YA RAFIKI ELIMU.
Uongozi wa Taasisi Ya RafikiElimu Foundation unapenda kuwahadharisha wananchi wote juu ya kuibuka kwa kundi la watu wanaofanya utapeli mitandaoni kwa kutumia jina la Taasisi ya RafikiElimu ( RafikiElimu Foundation.)
Siku ya Alhamiso ya jana tarehe 28 FEBRUARI 2013 mnamo majira ya saa 5 kamili asubuhi, ofisi yetu ilitembelewa na mwanadada aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA.
Mwanadada huyu baada ya kujitambulisha, aliomba kuonana na HUMAN RESOURCES MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu, baada ya kumuona alionesha fomu aliyopewa kupitia mtandaoni na watu waliojitambulisha kwake kama RafikiElimu Foundation.
Watu hao walitoa tangazo kupitia mtandao wa ZOOM TANZANIA wakidai kuwa wana wa- link, wahitimu mbalimbali wa vyuo vikuu na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali kwa ajili ya kufanya kazi katika taasisi hizo kama volunteers.
Mwanadada huyu akaendelea kueleza ya kwamba, baada ya kuona tangazo hilo alivutiwa na kutuma maombi ambapo walimjibu kwa kumpatia fomu aliyo takiwa kuijaza na kuirejesha kwao. Baada ya kujaza fomu hiyo, walimtumia barua pepe nyingine na kumwambia kwamba maombi yake yamekubaliwa, kisha wakamtumia fomu na kumwambia aijaze, aimbatanishe na CV yake, na kuwatumia pesa kiasi cha shilingi Elfu Tano ( TSh. 5,000/=) kwa njia ya MPESA kwenda namba 0763906931 (AMBAYO MBAYA ZAIDI, WAMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU).
Baada ya kuwatumia pesa hiyo, wakamwambia aripoti na fomu yake iliyojazwa na kuambatanishwa na CV kwa HUMAN RESOURCES MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu (ambaye kwenye barua hiyo walimtaja kama Mr. ALBERT EMMANUEL ) siku ya tarehe 28 FEBRUARI 2013 saa 5 kamili asubuhi.
Sisi Taasisi ya RafikiElimu tumeshangazwa sana na taarifa hii kwa sababu kwanza, hatukutoa tangazo la aina hiyo, lakini pili huwa hatuwatozi watu pesa ili kuwatafutia nafasi za kujitolea. Tumefadhaishwa sana.
Tumebaini kuwepo kwa utapeli unaofanywa na watu kwa jina letu, hivyo moja kwa moja tumekwenda kuripoti tukio hili la uhalifu katika kituo kidogo cha polisi kilichopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, sehemu ya Mlimani na kupewa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA MTANDAO. Tumelitazama tangazo hilo katika mtandao wa Zoom Tanzania. Tangazo hili lililowekwa mtandaoni mnamo siku ya tarehe 05 FEBRUARI 2013 lilisomeka kama ifuatavyo :
UDHAIFU WA TANGAZO HILI:
i. Namba waliyo weka haipo ( IT DOES NOT EXIST )
ii. Wanasema " We are looking for Highly motivated individuals to volunteer in differentprivate Organisation... (RafikiElimu Foundation, hatushughuliki na private organizations bali NON-GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS).
iii. Namba za simu walizo weka, hazipo kwenye blogu yetu.
iv. Katika tangazo lao, hakuna link inayo onyesha anuani ya blogu yetu.
v. Wametoa tangazo lao kwa lugha ya kiingereza, sisi kama RafikiElimu Foundation hatujawahi kutoa tangazo kwa lugha ya kiingereza.
vi. Kiingereza walicho tumia ni kibovu sana.
vii. Anuani ya barua pepe waliyo tumia ni batili na wala haipo kwenye taarifa zetu za kwenye blogu yetu. Anwani ya barua pepe waliyo tumia ni : graduatevolunteer@gmail.com wakati anuani ya barua pepe ya taasisi ya RafikiElimu Foundation ni : rafikielimutanzania@gmail.com
HATUA TULIYO CHUKUA BAADA YA KULIONA TANGAZO HILI NI KUUFAHAMISHA UONGOZI WA MTANDAO WA ZOOM TANZANIA, KUHUSU TANGAZO HILO LA KITAPELI ILI KUWANUSURU WANANCHI WENGINE ZAIDI NA TUNASHUKURU ZOOM TANZANIA WAMEPOKEA TAARIFA YETU NA KUAHIDI KULISHUGHULIKIA TATIZO HILO KWA KULIONDOA KATIKA TOVUTI YAO .
MAELEZO YA KWENYE FOMU YA MATAPELI HAWA

UDHAIFU WA FOMU HII :
1. Namba zao walizo zitoa kwenye fomu hizi za kitapeli, hazipatikani muda wote, wakati namba zetu zinapatikana muda wote.
2. Katika fomu yao ya kitapeli, hawajaandika location ya ofisi zilipo, hawajaweka sanduku la barua, blog adress wala namba za simu zinazo patikana.
3. Hakuna logo.
4. Hakuna sahihi.
5. Hakuna jina
6. Hakuna muhuri.
Tulipo jaribu kuwapigia kwa namba walizo ziweka kwenye mtandao ambazo ni +255 22 524 3785 tukajibiwa ya kwamba namba hizo hazipo ( the number your dialing are not existing ).
Na tulipo jaribu kuwapigia kwa namba 0763906931 nazo zikawa hazipatikani muda wote.
Taasisi yangu kwa kushirikiana na jeshi la polisi, tunafanya msako mkali dhidi ya mtu ama watu hawa na tunaahidi ya kwamba tutawakamata ndani ya muda ambao si mrefu sana na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
OMBI: Kama na wewe ni miongoni mwa walio tapeliwa na watu hawa, tafadhali wasiliana nasi kwa simu 0782405936 ili tushirikiane katika kuhakikisha wahalifu hawa wanatiwa mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
TAMKO LETU : Tunalaani vikali kitendo kilicho fanywa na ama kinacho fanywa na wahalifu hawa, kwani mbali na kuiba pesa za Watanzania masikini kama wao, kitendo hiki kinachafua jina la Taasisi yetu ambayo inafanya kazi zake kwa kushirikiana na wananchi.
ANGALIZO KWA WANAOTAFUTA KAZI :
i. Unapo tuma maombi ya kazi katika sehemu yoyote ile halafu ukaambiwa utume pesa ili kupatiwa kazi hiyo, jua kwamba huo ni utapeli na kazi hiyo haipo.
ii. Hakikisha unazifahamu ofisi za taasisi hiyo zilipo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yanayo husisha pesa.
iiii. Ni vyema kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kama taasisi hiyo kweli ipo.
iv. Unapoona tangazo la kazi, na kuvutiwa nalo, jitaidi kuwapigia simu walioweka tangazo na kuwauliza maswali mawili matatu kuhusu kazi hiyo.
HATA HIVYO: Tunashukuru kuwa mpaka sasa ni mtu mmoja tu ndie aliyeripoti kutapeliwa na watu hao kwa jina la Taasisi yetu. Hii ina maana kuwa Watanzania wengi wameelimika kwa sasa, inawezekana watu wengine walilishitukia tangazo hili na kuachana nalo.

0 comments:
Post a Comment