SETI YA MASHINE YA ULTRASOUND YENYE THAMANI YA SH 25 MILIONI
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya X-RAY Daktari Alban Ndekeye kulia na Daktari Paul Henry wa kitengo cha idara ya X-RAY wakati wa uzindua wa mashine ya ultrasound mpya yenye thamani ya sh25 milioni kwa ajili ya hospita ya rufaa ya mkoa Morogoro. Picha JUMAMTANDA.BLOG
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullazziz Abood kizungumza jambo kabla ya kuzindua mashine hiyo, kulia ni
Dk Ritha Lyamuya
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Godfrey Mtei akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo, kutoka kulia ni Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Rutha Lyamuya na mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullazziz Abood.
Mkuu wa Idara ya X-RAY Daktari Alban Ndekeye akizungumza jambo kuhusu mashine hiyo.
Sehemu ya viongozi wa idara mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
WAANDISHI wa habari Lilian Lucas na Josephine Malango.
NA LILIAN LUCAS, MOROGORO.
HOSPITALI ya rufaa ya mkoa wa Morogoro imepata mashine ya kipimo cha Utra-Sound yenye
thamani ya shilingi 25 milioni baada ya zaidi ya miezi miwili kutokuwa
na huduma ya mashine hiyo kwa wananchi ya mkoa wa Morogo.
Akizindua
mashine hiyo hospitalini hapo jana mbunge wa jimbo la Morogoro mjini
Abdulazizi Abood aliwataka watumishi wa idara ya utra-sound na x-ray
kutoa huduma kwa usawa kwa wananchi kwani kumekuwa na malalamiko ya mara
kwa mara kutoka kwao.
Aboodi
alisema huduma hiyo ni moja ya huduma zinazotegemewa na wananchi walio
wengi,na kwamba katika kipindi hicho cha miezi miwili wananchi walikuwa
wakipata huduma hiyo nje ya hospitali kwa gharama kubwa ambayo baadhi
yao walikuwa wakishindwa kulipia gharama hiyo.
“Naupongeza uongozi wa hospitali hii kwa kuona umuhimu wa kununua mashine hii kwani
nilikuwa nikipata malalamiko kutoka kwa wananchi wangu kwa jinsi
wanavyosumbuka pale anatakiwa kupiga Utrasound,”alisema Abood.
Baada
ya kuzinduliwa kwa mashine hiyo mbunge huyo alitoa mashine ya
kudurufu(printer) yenye thamani ya shilingi 500,000 ili iliwe kusaidia
katika kudurufu mara wanapomaliza kufanya vipimo kwa mgonjwa na kuahidi
kusaidia kupata mashine nyingine ya Utra-sound.
Akizungumza
katika uzinduzi huo mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa
Morogoro Dk Ritha Lyamuya alisema kuwa kupatikana kwa mashine hiyo
kutasaidia kupata majibu kwa usahihi ya wagonjwa watakaopata huduma hiyo.
Dk Lyamuya alisema kuwa mashine hiyo imekuwa ikipima watu 600 hadi 800 kwa mwezi na kwamba kipimo hicho hasa ni muhimu kwa wamama wajawazito na kimekuwa hakina malipo yeyote.
“Magonjwa
yanayotumika kupima katika mashine hii ni Moyo,kizazi ,kongoshi,ini,na
figo na kilipokuwa hakipo wananchi wetu walipata shida kutokana na
gharama wanazotozwa katika hospitali nyingine,”alisema Dk Lyamuya.
0 comments:
Post a Comment