Kwa ufupi
“Kinachotusikitisha ni kwamba pamoja na kasi hiyo ya
mauaji, ni kesi nne tu ndizo zilisikilizwa mahakamani na kutolewa
uamuzi. Sisi haturidhiki na kasi ya kusikiliza kesi za mauaji ya wenzetu
wenye albinism,” alisema ofisa uhusiano wa shirika hilo Kondo Seif.
http://www.freemedia.co.tz
WATU 73 wenye ulemavu wa ngozi (albino), wameuawa kwa nyakati
tofauti katika kipindi cha miaka sita iliyopita kuanzia mwaka 2007,
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Under the Same Sun (UTTS),
limeeleza.
Shirika hilo lilitoa takwimu hizo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka minne tangu kuanzishwa kwake. Under the Same Sun, ilianzishwa nchini mwaka 2008 na kusajiliwa rasmi Aprili 6 mwaka 2009.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa
washirika hilo walisema kuwa mbali na mauaji hayo, watu wengine 34
wamejeruhiwa kwa kukatwa viungo mbalimbali vya miili yao, ikiwamo mikono
na vidole, huku makaburi 19 yakifukuliwa kutafuta viungo vya wengine
waliouawa na kuzikwa.
“Kinachotusikitisha ni kwamba pamoja na kasi hiyo
ya mauaji, ni kesi nne tu ndizo zilisikilizwa mahakamani na kutolewa
uamuzi. Sisi haturidhiki na kasi ya kusikiliza kesi za mauaji ya wenzetu
wenye albinism,” alisema ofisa uhusiano wa shirika hilo Kondo Seif.
Kondo alisema Under the Same Sun imekuwa ikikutana
na changamoto nyingi katika utendaji wake wa kazi ikiwamo jamii
kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu.
0 comments:
Post a Comment