BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YAPIGA MARUFUKU WALIMU KUTUMIA WANAFUNZI KUSAHIHISHA MADAFTARI.


  • KUONGEZEKA idadi ya wakaguzi wa shule yapiga Marufuku Walimu Kutumia Wanafunzi Kusahihisha Madaftari ya Wanafunzi Wenzao.
  •  
 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha ukgauzi wa shule ili kuhakikisha ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya wanafunzi na ufundishaji shuleni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Marystella Wassena katika mahojiano na kituo cha Redio Uhuru cha jijini Dar es salaam.

Wassena amesema chini ya utaratibu na mfumo wa sasa kila shule inatakiwa kukaguliwa mara moja kila mwaka hatua ambayo imekuwa ikitekelezwa na wakaguzi wa elimu wa kanda na wa wilaya katika kuhakikisha maendeleo ya mwanafunzi. Hata hivyo  bado kuna changamoto katika  kuzifikia shule zote.

Mkurugenzi huyo amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa wakati, Wizara inakusudia kutumia mbinu na mikakati mbalimbali ili kuongeza kiwango cha ukaguzi shuleni ikiwemo kuongeza idadi ya wakaguzi.

“Kila shule inapaswa kukaguliwa mara moja kwa mwaka na tumekuwa tukifanya hivyo ingawa tumeona kwamba kuna haja ya kuongeza kiwango cha ukaguzi na kwa sasa kuna mipango inafanyika ili kuwezesha jambo hili  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.”Alisema Wassena.  

Amesema zipo nchi ambazo shule zinakaguliwa zaidi ya mara moja kwa mwaka. Alitolea mfano wa nchi ya Korea ya Kusini ambapo shule zinakaguliwa mara moja kila muhula, mfumo ambao amesema unaweza pia kutekelezwa Tanzania.

Ametaja baadhi ya juhudi ambazo Serikali inazifanya kwa hivi sasa ni kuimarisha ukaguzi wa shule kwa kushirikiana na UNICEF kutoa mafunzo kwa Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule ili washiriki kikamilifu kukagua shule zao ikiwa ni pamoja na ufundishaji na kuona kuwa mazingira ya shule zao yanafaa katika kutoa Elimu bora. 

“Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule watasaidia sana iwapo kila  mmoja wao atakuwa na ujuzi wa kukagua shule zao na kufahamu namna bora ya kuondoa mapungufu yanayojitokeza kwa kuwa wao wapo karibu zaidi na shule hizo,” alisema. 

Wassena ameeleza zaidi kuwa kumekuwa na juhudi nyingi za kuboresha ufundishaji shuleni, juhudi ambazo zimekuwepo hata kabla ya matokeo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012 amabazo ana imani kuwa zitatoa
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: