BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TANZANIA NI DHAIFU KATIKA KULINDA RASILIMALI ZAKE.

MWANANCHI.
DAR ES SALAAM
TAASISI moja ya masuala ya mapato imetoa ripoti yake ya mwaka 2011/12 kuhusu Utendaji na Utawala katika rasilimali. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Tanzania ni dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake ikishika nafasi ya 27 kati ya nchi 58 zenye usimamizi mbovu katika sekta hiyo.
Ripoti ya taasisi hiyo Revenue Watch Institute, inaeleza kuwa Tanzania iliyo na madini ya shaba, fedha, almasi na gesi asilia, imeshindwa kulinda na kud
hibiti rasilimali zake, hivyo kuathiri utendaji katika sekta nyingine.
Inaeleza kuwa katika masuala ya kisheria kuhusu madini Tanzania imeshika nafasi ya 46 kati ya nchi 58, ambayo ni sawa na asilimia 44 na kufafanua kuwa hali hiyo imetokana wananchi wake kutojua mambo mengi kuhusu rasilimali zao hali inayochangiwa na kutokuwa na sheria huru ya vyombo vya habari.
“Kingine ni Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mamlaka ya Mapato (TRA), zote kukusanya malipo kutoka katika kampuni za madini. Kampuni hizo pia hufanya baadhi ya malipo moja kwa moja kwa wananchi walioathirika, vinginevyo mapato yote huenda Hazina,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Inaeleza kuwa baada ya miaka mingi ya Tanzania hupata mrabaha mdogo kutoka katika kampuni za madini, mwaka 2010 sheria ya madini ilifanyiwa marekebisho na mrabaha kuongezwa, lakini bado mikataba ya kampuni za madini imeendelea kuwa siri.
Inaeleza kuwa kampuni hizo zinatakiwa kueleza athari za mazingira katika migodi, lakini nyingi hazifanyi hivyo na kwamba hali hiyo ni kinyume na matakwa ya leseni zao.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kampuni hizo zinatakiwa kuweka wazi taarifa zake za mapato kwa kuwa mwaka 2012, Tanzania ilitia saini mpango wa uwazi katika shughuli za madini.
Inaeleza kuwa sababu ya Tanzania kuwa na usimamizi mbovu katika sekta ya madini ni pamoja na kushindwa kuchapisha mikataba ya madini wala kuwa na takwimu za kampuni zinazomilikiwa na Serikali, licha ya kuwa inatoa baadhi ya taarifa juu ya uzalishaji na mapato ya madini.
“Wizara ya Fedha huchapisha habari juu ya kiasi cha uzalishaji na thamani ya mauzo ya nje, lakini haitoi maelezo juu ya mapato katika madini,” inasema sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza.
“Wizara ya Nishati na Madini inachapisha maelezo kuhusu hifadhi, kiasi cha uzalishaji, bei ya kuuza nje, idadi ya kampuni, kodi na mirabaha, lakini haitoi takwimu juu ya ada ya leseni, gawio au mafao.”
Inafafanua kuwa licha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) huchapisha ripoti kila mwaka kuhusu mauzo ya nje na kiasi cha uzalishaji, sheria mpya ya madini haijaondoa mamlaka ya hiari ya Waziri wa Nishati na Madini katika utoaji leseni na mazungumzo ya mkataba.
Inaeleza kuwa Tanzania pamoja na kuwa na mazingira mazuri imepata alama za chini katika utawala wa sheria, hali inayotokana na kuwepo kwa vitendo vya rushwa na uwajibikaji mdogo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: