MOJA YA BASI LA TAQWA LIKIWA LIMEPATA AJALI
MKOANI MOROGORO. PICHA NA MAKTABA
JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
ABIRIA saba waliokuwa
wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 273 CDR kutoka
jijini Dar es Salaam kwenda Malawi wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20
kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jioni jana katika eneo la Nyololo
wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
mmoja kati ya
mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Dkt Matatala alisema kuwa ajali hiyo
imetokea JANA mida ya saa 11 jioni wakati basi hilo likitokea Dar es Salaam
kwenda
nchini Malawi.
nchini Malawi.
Alisema
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T 104 DZZ ambalo
lilikuwa likitokea Makambako kuelekea Iringa,lori lililokuwa likijaribu
kulipita lori len
ye namba za usajili T 227 AVC na kushindwa kupita na kuishia
kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo pia lilikuwa likija kwa mwendo wa
kasi.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea katikati ya
mji wa Nyololo ambapo ni jirani kabisa na eneo lenye matuta ya kuzuia magari
kwenda kwa mwendo kasi.
Alisema kuwa hadi
majira ya saa 12.45 jioni maiti tano zilikuwa zimetolewa katika basi hilo la
Taqwa na kuwa jitihada za wasamaria wema kutoa maiti na majeruhi katika eneo
hilo zimeendelea kufanyika.
Mbali ya maiti hizo pia
alisema jumla ya majeruhi 20 waliokolewa na kukimbizwa katika Hospitali ya
wilaya ya Mufindi kwa matibabu zaidi. Dkt Matatala alisema kuwa katika tukio
hilo wananchi wameweza kuimarisha ulinzi zaidi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja
na kulinda mali za majeruhi na abiria waliopoteza maisha yao kwa ajili
hiyo.
Wakati huo huo wananchi wa
eneo hilo la Nyololo wameelekeza lawama zao kwa jeshi la polisi wilayani
Mufindi kwa kuchelewa kufika katika eneo la tukio na kuwa taarifa wamepewa
mapema ila hadi majira ya saa 12.50 hakukuwepo na askari aliyefika eneo hilo.
Hii ni ajali ya pili kutokea
katika wilaya ya Mufindi kwa kipindi cha wiki moja baada ya ajali nyingine
mbaya kama hii kutokea eneo la Mafinga kwa gari ndogo iliyokuwa ikiendeshwa na
paroko wa kanisa katoliki Ifunda marehemu Alfonce Mhamilawa kutokea kwa kuingia
nyuma ya lori.
0 comments:
Post a Comment