KATIKA
kile kinachoonekana kwamba ni wizi mtupu, baadhi ya vijana wanaojifanya kutunza
Makaburi ya Kinondoni wamebuni njia ya kuwaibiawatu kwa kutumia kaburi la nguli
wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba.
Vijana hao hujipatia kipato kwa
kuwatoza watu wanaofika makaburini hapo shilingi 5,000 kwa ajili ya kuliona na
kupiga picha na kaburi la nguli huyo.
Utafiti uliofanywa na Risasi
Jumamosi umebaini kwamba wageni wanaotoka nje ya Dar ndiyo wanaoongoza kwa
kulizwa zaidi.
Sosi wetu
ambaye naye alilizwa, alisema kuwa alishangazwa kwa kutozwa fedha na
vijana hao lakini hakuwa na budi kufanya hivyo yeye na wenzake ili
kutimiza lengo la kulitembe
lea kaburi hilo la kipenzi chao.
Baada ya kupata
habari hizo, gazeti hili liliunda kikosi kazi cha waandishi wake na kwenda
kuwanasa vijana hao.
WAANDISHI WATINGA MAKABURINI
Alhamisi iliyopita, waandishi wetu walifika katika Makaburi ya
Kinondoni na kukutana na jamaa kibao waliokuwa wakijishughulisha na kazi za
ujenzi wa makaburi na kupanda maua ambapo walimchagua mmoja wao
aliyejitambulisha kwa jina la Mdenmark ili kuongea na wageni nao.
WAPANGA
DAU
Baada ya kuwaita chemba, jamaa huyo alianza kuwapiga somo
waandishi wetu na kuwaambia kwa kuwasaidia wampe shilingi 5,000 ili kuwaonesha
kaburi na kuwapa historia ya marehemu tangu enzi za uhai wake mpaka alipokutwa
na umauti huku akiwatahadharisha wafanye jambo hili kuwa siri.
MCHEZO WAMALIZWA
Baada ya kukubaliana kiasi hicho cha fedha, waandishi walimpatia
Mdenmark kiasi cha fedha na akachukua jukumu la kuwapeleka mahali lilipo kaburi
hilo.
Wakiwa kaburini kwa Kanumba, waandishi wetu kwa kutumia ustadi
mkubwa walifanikiwa kumpiga picha tapeli huyo akiwaelekeza mambo kadhaa juu ya
marehemu na picha nyingine zikimuonesha akipokea fedha kutoka kwa waandishi.
TAMKO
LA MHARIRI
Si
sawa kulipa fedha kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba, mara kadhaa waandishi
wetu wamemsikia mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa akisema kuwa
hafahamu mradi huo.
Ni
jukumu la Jeshi la Polisi chini ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
DCP Suleiman Kova kuwanasa wajanja hao.
0 comments:
Post a Comment