Jana
ilifanyika Mechi ya watani wa jadi hapa jijini Dar es salaam, katika
uwanja wa taifa na haya ni matukio ambayo sisi tuliona ni muhimu
waliokosa kwenda kushuhudia mechi wasiyakose, hawa walikuwa watani wa
jadi, mbwembwe zao silidumu kwa dakika nne tu.
Ilituchukua muda kugundua kilichokuwa kimebebwa kwenye ungo, we unahisi nini?
Huyu jamaa eti alijifanya yeye ni Simba, kakubali kuolewa na Bwana Yanga, cheki maandishi yake mgongoni.
Kuna wakati Kaseja alizuia shuti, likamgonga kichwani akaanguka, akaangalia kwanza...
...akarudi chini kus'kilizia
Watu hao.
Utani ulikuwepo pia.
Yote kwa yote mechi iliishia Yanga 2, Simba 0
Hii hiyo ni mechi ya 101 kwa timu hizo kukutana katika michuano
mbalimbali, na kati ya hizo, Yanga ilishinda mara 38, Simba mara 32,
huku mara 31 zikitoka sare.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig alikubali matokeo na kusema, Yanga
walistahili ushindi kwa vile kikosi chao kilikuwa bora kulinganisha na
kikosi chake ambacho, amesema kina miezi miwili tu tangu akitengeneza
upya.
Picha na Emanuel Herman wa Mwananchi
Picha na Emanuel Herman wa Mwananchi
0 comments:
Post a Comment