Tembo wakijitafutia chakula katika moja ya mbuga za wanyanya zilizopo nchini Tanzania.
DAR ES SALAAM.
KUSHAMIRI kwa vitendo vya ujangili nchini kumeifanya Tanzania kutajwa kuwa moja kati ya nchi nane zinazoongoza katika biashara haramu ya pembe za ndovu huku pia nchi za Kenya na Uganda zikitajwa.
Katika mkutano wa Kimataifa wa Biashara kwa Viumbe
Vilivyopo Hatarini Kutoweka (CITES) uliofanyika Bangkok, Thailand,
mwezi Machi mwaka huu, Tanzania ilitajwa kuwa ni miongoni mwa nchi nane
zilizo mstari wa mbele katika biashara ya pembe za ndovu.
Nchi hizo ambazo zinatambuliwa kama kundi la
wanane ‘gang of eight’ ni pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda, ambazo
zimewekwa katika kundi la nch
i zinazozalisha pembe hizo. Nchi zilizowekwa katika kundi la wanunuzi ni China na Thailand, Malaysia, Vietnam na Ufilipino.
i zinazozalisha pembe hizo. Nchi zilizowekwa katika kundi la wanunuzi ni China na Thailand, Malaysia, Vietnam na Ufilipino.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Profesa Alexander Songorwa amethibitisha kupelekwa
kwa ripoti hiyo, lakini akakataa kuyataja mapendekezo yaliyomo kwenye
ripoti kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia masuala hayo kwenye simu na
kumtaka mwandishi kwenda ofisini kwake Jumatatu.
“Ni kweli tumepeleka ripoti hiyo CITES, lakini
siwezi kuizungumzia, zaidi nakuomba uje ofisini kwangu siku ya Jumatatu
nitakufafanulia,” alisema Songorwa.
Alipopigiwa simu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Khamis Kagasheki alimtaka mwandishi kumpigia baada ya saa moja, lakini
alipopigiwa tena simu yake ya mkononi haikupokewa.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na CITES kupitia
mtandao wake mwishoni mwa wiki, inaitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa
nchi nane zilizowasilisha ripoti inayoeleza namna itakavyotokomeza
biashara ya pembe za ndovu.
Awali kamati ya CITES ilikuwa imeweka Machi 15, mwaka huu kuwa ni siku ya mwisho kwa nchi hizo kuwasilisha mipango yake.
Nchi nyingine zilizowasilisha mpango kazi ni
pamoja na Uganda, Kenya, Vietnam, China, Singapore, Malaysia, Ufilipino
na Thailand.
Katibu Mkuu wa CITES, John Scanlon alisema ripoti
ya kila nchi itapelekwa katika kamati maalum ambayo itafuatilia
mapendekezo yaliyotolewa kwa kuyafanyia kazi ikishirikiana na nchi
husika.
“Itakapofika Julai 2014, Sekretarieti itatoa
tathmini ya mapendekezo yaliyotolewa na kila nchi na namna
yalivyotekelezwa,” alisema Scanlon.
Akitoa hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara ya Utamaduni na Utalii kwa mwaka 2013/2014, Kagasheki, alisema
Wizara itaendelea kutekeleza mikataba na makubaliano ya kikanda na
kimataifa ukiwamo ule wa CITES.
0 comments:
Post a Comment