STAA mwenye swaga za kupitiliza Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amepatwa na
masaibu ya kutaka kushushiwa kipondo hevi na demu ambaye jina lake
halikupatikana mara moja baada ya kumpulizia pafyumu bila ridhaa yake.
Tukio hilo liloloonekana kumkosesha amani PHD, liliibuka Jumapili
iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, jijini Dar wakati staa
huyo alipokuwa akizindua singo yake mpya inayofahamika kwa jina la Rest
of My Life.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kilimtonya
paparazi wetu kuwa wakati staa huyo akipafomu jukwaani alishika pafyumu
kama swaga za kunogesha shoo huku akiwapulizia baadhi ya mashabiki wake,
haswa warembo.
Timbwili likiendelea.
“Aliwapulizia pafyumu baadhi ya warembo akiwa jukwaani lakini kumbe
kitendo kile hakikumpendeza mdada mmoja hivi aliyeonekana kama ni
shombeshombe.
“Sasa akaona isiwe tabu, akasubiri aliposhuka
jukwaani, akamfuata nyuma ya jukwaa (back stage) na kuanza kumshika
shati huku akihoji kwa nini alimpulizia pafyumu hiyo bila ridhaa yake,”
kilisema chanzo hicho.
Wadau wakijaribu kumtuliza dada huyo.
Wakati mwanadada huyo akiwa amemtaiti PHD, baadhi ya watu waliokuwa
karibu waliingilia kati na kumsihi dada huyo apunguze munkari, zoezi
ambalo lilichukua takriban robo saa.
Hemed alifanikiwa kuchomoka kwenye himaya ya mlimbwende huyo na kumwacha akiendelea kumchimba biti.
Juhudi za kumpata Hemed juzi Jumanne ili aeleze kwa undani kilichompata
hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.
SOURCE:GPL




0 comments:
Post a Comment