
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imefuta hukumu ya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Saalam, iliyomuachia huru mkurugenzi wa kampuni ya Richmond
Ltd, Naeem Adam Gire, limeandika gazeti la Tanzania Daima la leo
Gire alikuwa akikabiliwa na makosa ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za
uongo na kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa umma.
Hukumu hiyo ilitolewa kutokana na rufaa Na.126/2001 iliyokatwa na
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi(PICHANI) dhidi ya uamuzi wa
kesi ya kutoa taarifa za uongo kwa Shirika la Umeme la TANES
CO Na. 15/2009
iliyokuwa ikimkabili Gire ambapo mwaka juzi Hakimu Mkazi Waliarwande Lema
alimuona hana kesi ya kujibu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Lawrance Kaduri ambaye katika hukumu yake
hiyo alisema alisikiliza hoja za mawakili wa serikali waliokuwa wakimwakilisha
muomba rufaa (DPP), Frederick Manyanda na Oswald Tibabyekomya na mjibu rufaa
alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa.
“Baada ya kusikiliza hoja zote mbili na pia nimeangalia nakala ya hukumu
ya Mahakama ya Kisutu iliyomuachia huru Gire kwa maelezo kuwa hana kesi ya
kujibu.
“Mahakama hii imefikia uamuzi wa kuufuta uamuzi huo kwa sababu imebaini
kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha ulioletwa na upande wa jamhuri kule katika
Mahakama ya Kisutu ambapo umejitosheleza kumfanya Gire apande kizimbani na
aanze kujitetea,” alisema Jaji Kaduri.endelea kupitia na kukopi
audifacejackson blog.Jaji Kaduri alisema anakubaliana na hoja za wakili
wa Tibabyekomya iliyodai kuwa Hakimu Lema alikosea kisheria katika uamuzi wake;
alisema kuwa kosa la kughushi limeshindwa kuthibitika, uamuzi ambao jaji huyo
alisema hakimu Lema alisema alitumia sheria ambayo ilishapitwa na wakati kwa
kusema kosa la kughushi limeshindwa kuthibitika.
Alisema kwa mujibu wa hati ya mashtaka kosa hilo la kughushi, Gire
anadaiwa kulitenda Machi 13, 2006 Dar es Salaam, kwa nia ovu; alighushi nguvu
ya kisheria ya Machi 13, 2006 kwa lengo la kuonyesha Mohamed Gire ni Mwenyekiti
wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ya Texa America.
Aliongeza kuwa Gire alisaini hati ya nguvu ya kisheria inayompa mamlaka Naeem
Adam Gire (mjibu rufaa) wa hapa jijijini kuendelea na shughuli za kibiashara za
kampuni hiyo hapa nchini kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 335(d) (iii) cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
“Hivyo basi mahakama hii inakubaliana na mawakili wa mwomba rufaa (DPP),
kuwa kosa hilo la kughushi hati ya nguvu ya kisheria liliweza kuthibitishwa na
upande wa jamhuri hivyo mahakama hii inatamka wazi Hakimu Lema alikosea
kisheria kusema upande wa jamhuri ulishindwa kuthibitisha kosa la kughushi hati
ya nguvu za kisheria na kuwasilisha nyaraka hizo ambazo zilighushiwa kwa
maofisa wa umma kwa lengo la kuonyesha kampuni hiyo ilikuwa na uwezo wa
kuzalisha umeme hapa nchini wakati si kweli ili ipewe zabuni,” alisema Jaji
Kaduri.
Aidha Kaduri alisema mahakama yake imejiridhisha kuwa kosa la kwanza na
la pili (kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo) limeweza kuthibitishwa na
upande wa jamhuri, hivyo mahakama yake inaamuru kesi ya msingi iliyokuwa
imemalizika kwa Gire kuachiliwa huru baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu,
irudi upya katika Mahakama ya Kisutu na Gire anaanze kujitetea.
Mwaka juzi, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliandware
Lema, alimwachilia huru Gire baada ya kumuona hana kesi ya kujibu na hakimu
huyo alikwenda mbali zaidi na kusema upande wa jamhuri uache kufungua kesi kwa
kukurupuka na kwamba mwisho wa siku mahakama inapowaachilia huru washtakiwa,
matokeo yake mahakama inakuja kubebeshwa lawama.

0 comments:
Post a Comment