MARIO Balotelli ameachwa na aliyekuwa mchumba Fanny Neguesha — siku
chache baada ya kuripotiwa kusema kwamba kikosi kizima cha Real Madrid
kingeweza kulala nae ikiwa wangeitoa Borussia Dortmund.
Mwanamitindo
Fanny, 22, aliondoka kwenye nyumba ya mshambuliaji huyo huko Italia
baada ya kugombana kutokana kutoelewana baina ya wawili hao.
Straika huyo wa AC Milan Balotelli, 22, alisema wachezaji wote wa Madrid — akiwemo Cristiano Ronaldo — wangeweza
kufanya mapenzi na demu wake Fanny ikiwa juzi wangeweza kufanya maajabu
ya kugeuza matokeo ya mechi ya kwanza (4-1) na kufanikiwa kwen
da Wembley.
da Wembley.
Balo alikaririwa na gazeti la Marca akisema: “Ikiwa Real Madrid
wataenda kucheza fainali ya Champions League, nitamtoa mchumba wangu
alale nao wote." Ingawa baadae alikana kutoa kauli hiyo.
Balotelli aliachana na mama wa mtoto wake wa kike mtangazaji wa
TV Raffaella Fico, 25, kisha ndio akaanzisha mahusiano na mwanamitindo
Fanny ambaye ana asili ya Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment