Kwa ufupi
Saa moja kabla ya Ambroce kupandishwa kizimbani
saa nne asubuhi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
aliitisha mkutano na waandishi wa habari kitendo ambacho kiliwafanya
baadhi yao kushindwa kufuatilia vyema tukio hilo.http://www.mwananchi.co.tzMtuhumiwa wa kurusha Bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Joseph,Parokia ya Olasiti ,Jimbo Kuu la Arusha,Victor Ambrose Calist
akiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya kusomewa mashtaka
21 ya kuua na kujaribu kuua.Picha Filbert Rweyemamu.
ARUSHA.
MTUHUMIWA mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni kuhusiana mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha na kusomewa masht
aka 21 yakiwamo ya mauaji na kujaribu kuua.
MTUHUMIWA mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni kuhusiana mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha na kusomewa masht
aka 21 yakiwamo ya mauaji na kujaribu kuua.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kamuzora, mtuhumiwa
huyo, Victor Ambrose (20), dereva wa Bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa
Mromboo, Arusha alisomewa mashtaka hayo yakiwamo matatu ya mauaji ya
watu watatu waliofariki katika tukio hilo lililotokea Mei 5, mwaka huu.
Wakisoma kwa kupokezana hati ya mashtaka, Mawakili
wa Serikali, Zachariah Elisaria na Haruna Matagane walidai Calist pia
anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo
kimyakimya akiwa chini ya ulinzi wa maofisa wa polisi na hakutakiwa
kujibu lolote kwa sababu mashtaka yanayomkabili yanapaswa kusikilizwa na
Mahakama Kuu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 27, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.
Saa moja kabla ya Ambroce kupandishwa kizimbani
saa nne asubuhi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
aliitisha mkutano na waandishi wa habari kitendo ambacho kiliwafanya
baadhi yao kushindwa kufuatilia vyema tukio hilo.
Waarabu waachiwa huru
Polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni
waliokuwa wakishikiliwa kuhusiana na tukio hilo baada ya uchunguzi
uliofanywa na Polisi wa Tanzania, Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI)
na Polisi wa Kimataifa (Interpol) na kubaini hawakuhusika.
Kamanda Sabas aliwaambia waandishi wa habari
ofisini kwake jana kuwa raia hao walikamatwa baada ya kutiliwa shaka
walipoonekana wakitoka kwenye hoteli moja karibu na Kituo Kikuu cha
Mabasi Arusha, muda mfupi baada ya tukio hilo.
Raia watatu wa Falme za Kiarabu(UAE), walioshikiliwa na kuachiwa wamegundulika kuwa ni watumishi wa Serikali.
Kamanda Sabas aliwataja kuwa ni Abdul Azziz
Mubarak (30), (Mamlaka ya Mapato), Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri
(29), (Zimamoto) na Daeed Abdulla Saad (28), ambaye ni Askari wa
Usalama Barabarani.
Raia hao pamoja na mwenzao, Al-Mahri Saeed Mohseen
(29) kutoka Saudi Arabia, walikabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji
kuchunguzwa iwapo waliingia nchini kihalali.
0 comments:
Post a Comment