BABA wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius
Nyerere, ni miongoni mwa Watanzania watatu wanaotarajiwa kutambuliwa na
kuenziwa na Umoja wa Afrika (AU) rasmi kama Mwafrika Mashuhuri wa
Kimaj
umui.
Hatua hiyo inatokana na kuheshimu
mchango wao katika mapambano ya Uhuru wa Afrika na kuanzishwa kwa Umoja
wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambao sasa unajulikana kama AU.
Watanzania wengine katika kundi hilo la
‘Mwafrika Mashuhuri’ ni Rashidi Kawawa na Sebastian Chale, Katibu Mkuu
wa Kwanza wa Sekretarieti ya Kamati ya Ukombozi wa OAU, ambao kwa sasa
ni marehemu.
Kutokana na mchango wa Nyerere katika
Umoja huo, mjane Mama Maria Nyerere amealikwa kuhudhuria sherehe za
miaka 50 ya Umoja huo uliozaliwa Juni 25, 1963, akiwa katika kundi la
wageni maalumu wa kimataifa na kikanda wa Bara la Afrika.
Wengine walioalikwa na kuwasili juzi
wakiwa sehemu ya ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya sherehe hizo
ni marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, wakiwa
miongoni mwa marais wote wastaafu wa Afrika walioalikwa.
Ujumbe wa Tanzania katika sherehe hizo
unawashirikisha pia Dk Salim Ahmed Salim, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja
huo kwa muda mrefu zaidi wa miaka 12 kuliko Katibu Mkuu mwingine,
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro na
aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya OAU kusini mwa
Afrika, Brigedia Jenerali Hashim Mbita.
Wakati wa uongozi wa Dk Salim, ndipo OAU ilipofanyiwa marekebisho na mabadiliko makubwa, kutoka OAU na kuwa AU.
Aidha, AU imealika watu mashuhuri
walioliletea Bara la Afrika heshima na sifa kupitia siasa, michezo,
muziki na uongozi wa jumuiya za Umoja huo, wakiwamo Watanzania, Getrude
Mongela ambaye alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Dk Rosebud
Kurwijila ambaye ni Kamishna Msaidizi wa Masuala ya Kilimo na Uchumi wa
Kamisheni ya AU, na Jenerali Ulimwengu ambaye alikuwa kwa miaka mingi
akiiwakilisha Tanzania katika Umoja wa Vijana wa Afrika mjini Algiers,
Algeria.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara ya Rais
Kikwete, jana alitarajiwa kushiriki Mkutano Maalumu wa Wakuu wa Nchi za
AU na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwa Umoja huo na leo
atahudhuria Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambao
umepangwa kuendelea kwa siku mbili.
0 comments:
Post a Comment