Waombaji
wa nafasi za kazi Serikalini kwa tangazo lililokuwa limetolewa tarehe
26 Machi, 2013 kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma ambalo mwisho wa kutuma maombi ilikuwa terehe 9 Aprili,
2013 wametakiwa kuangalia majina yao katika tovuti ya Sekretarieti ya
Ajira kuanzia tarehe 13 Mei mwaka huu ili kujua endapo wamechaguliwa kwa
ajili ya kufanya usaili wa nafasi walizoomba.
Naibu
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili amesema ofisi yake
imepokea jumla ya barua za maombi ya kazi 20,763 ambazo mchanganuo wake
kwa tangazo la Kiingereza imepokea barua za maombi 6,332 na kwa tangazo
la Kiswahili imepokea barua za maombi 14,431 ambapo Ofisi yake iko
katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi wa maombi hayo ili
kuweza kuendelea na zoezi la usaili.
Mrumapili
amebainisha kuwa kwa tangazo la Kiingereza lililokuwa na nafasi wazi
185 ni kwa ajili ya Waajiri kutoka katika Taasisi za Umma zifuatazo;
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO), Chuo Kikuu Mzumbe
(MU), Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Wakala wa Mkemia Mkuu wa
Serikali (GCLA), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania
(TFNC), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Taasisi ya
Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Chuo
cha Mafunzo ya Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia
Mbeya (MUST), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Shirika la Utafiti na
Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG),
Amewataja
Waajiri kuwa ni pamoja na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Wakala wa
Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA), Kituo cha zana za Kilimo na Ufundi
Vijijini (CAMARTEC), Chuo cha Maji (WDMI), Chuo cha Mipango
Dodoma(IRDP), Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC), Taasisi ya
Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI), Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa Muhimbili
(MOI), Chuo cha Bandari Dar es Salaam (DMI), Wakala wa Mafunzo ya
Uongozi wa Elimu (ADEM), Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Wakala wa Serikali Mtandao (eGA),
Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Chuo cha Diplomasia na
Uhusiano wa Kimataifa (CFR).
Amesema
kwa upande wa Tangazo la Kiswahili lilikuwa na nafasi wazi 949 ambapo
Waajiri wake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha, Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa
Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia
na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi
na Technolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba
na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili,
Wengine
ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza,
Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara,
Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa,
Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.
Nafasi
nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi,
Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo,
Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema,
Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala,
Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli,
Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora,
Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino,
Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri
ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
Aidha,
amewataka waombaji na wadau wengine kurejea Matangazo ya nafasi za kazi
yaliyokuwa yametolewa tarehe 26 Machi, 2013 ili kujikumbusha kuhusu
nafasi husika zilizokuwa zimetangazwa.Alimalizia kwa kusema kuwa
waombaji ambao hawataona
majina
yao pindi majina yatakapotangazwa wajue hawakufanikiwa kutokana na
kutokukidhi vigezo vya tangazo kwa nafasi husika walizokuwa wameomba,
hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi hizo
zitakapotangazwa tena.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 30 Aprili, 2013.
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz au Simu; 255-687624975
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment