WANAFUNZI
WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI MWERE MANISPAA YA MOROGORO WAKIFANYA
MTIHANI WA TAIFA WA SOMO LA HISABATI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA
2012.
PICHA JUMAMTANDA.BLOG
SEKTA ya elimu nchini imekuwa ikipigiwa kelele na jamii kutokana na namna ya muundo wake na namna bora ya ufundishaji wa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na hata elimu ya juu.
Moja katika mabadiliko yanayotakiwa kuangaliwa kwa kina na jamii ni hatua ya kukosekana kwa misingi bora ya kujisomea kwa wanafunzi wetu ikiwemo vitabu na makala mbalimbali kuanzia ngazi ya familia hadi elimu ya juu kwani hii inaweza ikawa ni moja ya chanzo cha umaskini wa kufikiri na ubunifu katika kazi miongoni mwa wasomi wetu hapa nchini Tanzania.
Tatizo kubwa la elimu lililopo ni matokeo mabovu ya misingi ya elimu tangu katika ngazi ya familia miongoni mwa Watanzania walio wengi ambapo wengi wao hawana tabia ya kujishughulisha na usomaji wa vitu mbalimbali ikiwa ni pam
oja na vitabu, hivyo kushindwa hata wao wenyewe kujiwekea mipangilio mizuri na vipaumbele vya maisha yao na watoto wao.
Suala la watu kujenga tabia ya kusoma vitabu ni moja ya mafanikio ameeleza kuwa kila mafanikio huanza kama wazo ambalo huboreshwa kupitia kusoma vitu vitabu na makala mbalimbali hivyo kumsaidia mtu kupata maarifa zaidi na ubunifu wa kumuwezesha kufanya kitu kikubwa kitakachodumu kwa muda mrefu zaidi.
Ni wazi shughuli yoyote ambayo hutumia nguvu zaidi kuliko akili matokeo ya shughuli hiyo hua ni ya muda mfupi tofauti na shughuli ambayo hutumia akili zaidi na nguvu kidogo ambapo mafanikio yake hua ni makubwa na ya muda mrefu na faida kwa watu wengi zaidi.
kuna idadi kubwa ya watu wengi wanaishi maisha yasiyo na vipaumbele, lakini dhamira zao huwashtaki na hata kuwaonya kurudi kwenye misngitra bora ya kuweza kufikia lengo.
Changamoto kubwa inayowakabili watu wa aina hiyo ni kukosa chombo cha kuwahamasisha katika kufanya mabadiliko hayo ya maisha yao , hivyo kupitia kazi za maandishi ikiwa ni pamoja na kusoma vitabu mtu anaweza kupata hamasa na nguvu katika kufanya mabadiliko ya maisha yake kwa kuweka vipaumbele vyenye tija katika ya sasa na ya baadae.
Hata hivyo hatua ya Serikali iliyotangwazwa hivi karibuni kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo ya kurudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma haiwezi kuwa njia ya kufikia safari ndefu ya kufanya maboresho katika sekta hiyo mtambuka.
Naibu Waziri Mulugo alisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji. Kwamba wasipotandikwa mambo hayaendi.
Ni kweli kama alivyosema kuwa watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao.
Pamoja na kuelekeza lawama kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na haki za binadamu, akidai kuwa yamekuwa yakipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo shuleni na kusababisha kushuka kwa nidhamu kwa kiasi kikubwa.
Sawa hizi zinaweza zikawa ni hoja madhubuti kwake au kwa Serikali lakini kwa kufanya hivyp ndio tutakuwa tumeweka misingi imara ya elimu yetu nchini, ikiwa kila mmoja wetu kwa kuanzia kwa viongozi wataihamasisha jamii kufanya mabadiliko chanya ni nwazi tunaweza kufikia lengo.
Nachelea kukubaliana na msimamo huo wa serikali alioutangaza Mulugo kwani hilo si suluhisho la matokeo mabaya ya mitihani yanaojitokeza kila mwaka nchini.
Kutokana na hali hiyo niona bado Tanzania yetu ina safari ndefu wa kuelekea kuweka mazingira bora ya elimu kwa kuwa na miundombinu ya kisasa, pamoja na vifaa vya kufundishia kama njia ya kurudisha ari kwa wasomi wetu na wataalamu wetu wa baadae.
Mungu Ibariki Tanzania. http://www.mtanzania.co.tz
0 comments:
Post a Comment