JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni limewatia mbaroni watu wanne akiwamo
wakili wa kujitegemea kwa kujihusisha na mtandao hatari wa utapeli wa
kuuza viwanja vya watu. Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela (Pichani) alisema watu hao hutumia nyaraka bandia kuonyesha kuwa nyaraka hizo ni halali na zimetolewa na Wizara ya Ardhi.
“Watuhumiwa hawa ambao majina yao tumeyahifadhi kwa ajili ya mahojiano tuliwakamata Mei 15 mwaka huu eneo la Morocco,” alisema Kenyela.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa karibu na jengo la Airtel baada ya kutaka kumtapeli raia wa a China kwa kumuuzia kiwanja kilichoko Masaki chenye tham
ani ya dola za Marekani 500,000 huku wakati kiwanja hicho siyo mali yao.
Alisema mmiliki halali wa kiwanja hicho amepatikana na kuonyesha nyaraka halali za umiliki wa kiwanja hicho.
Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia ofisi ya wakili wa kujitegemea kuandaa mikakati yao ya utapeli, alisema.
Alisema watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Kamanda Kenyela alisema raia 12 wa kigeni kutoka Ethiopia wamekamatwa kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.
Alisema a watuhumiwa hao walikamatwa kati ya Mei 2 na 6 katika maeneo ya Kimara mwisho, Tegeta Kibaoni na Kawe.
“Walipohojiwa walidai waliingia Tanzania kupitia Kenya wakiongozwa na Mtanzania, Shenuru Mbelwa (28), dereva wa gari hilo mkazi wa Mbagala Charambe,”alisema Kenyela.
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Binamu Demeke(24), Mihyetu Elias (18), Aminiel Takata (22), Meles Elisido(22), Meles Lubebo (26), Wondimu Shamango(24), Zewde Nuramu (26) na Meleku Kebed(25).
Wengine Tegese Eliasi (20), Abise Abuye(29), Yona Alex (19) na Egu Damasi.
Wakati huohuo jeshi la polisi Mkoa wa Kinondoni katika miezi sita liliwakamata watuhumiwa 716 kati yao wanawake 678 na wanaume 38 kwa kufanya biashara haramu ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya ushoga.
CHANZO http://www.mtanzania.co.tz

0 comments:
Post a Comment