Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda |
WATU 10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa
za kulevya katika kipindi cha miaka mitano pekee na kuonyesha namna
gani biashara ya dawa hizo lilivyo tatizo nchini.
Pinda alisema kumekuwa na wimbi kubwa la
Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani
na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Aidha, amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
“Vile vile katika kipindi hicho jumla ya
Watanzania 240 walikamatwa katika nchi mbalimbali, zikiwamo Brazil,
Pakstani na Afrika Kusini,” alisema Pinda.
Alisema hali hiyo imekuwa ikiharibu
taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata
usumbufu, masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali
duniani.
Pinda alisema hali hiyo inatokana na sifa mbaya inayojengeka kwa Watanzania wanaosafiri katika nchi hizo.
Alisema zipo dalili kwamba, endapo
biashara hiyo itaachwa iendeleee, athari zaidi, zikiwamo kuingiliwa kwa
misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa kwa manufaa binafsi,
kuongezeka kwa waathirika wa rushwa.
Aidha, alisema uwapo wa biashara hiyo
huongeza mzunguko wa fedha haramu na kusababisha mfumko wa bei na hivyo
kuongeza hali ya umaskini.
Pinda alisema kwa mujibu wa vyombo
vya dola, takwimu zinaonyesha viwango vya Heroin na Cocaine
zinazoendelea kukamatwa nchini, kuanzia mwaka 2000 ni vikubwa kuliko
vile vilivyokamatwa miaka 10 iliyopita.
Alisema mwaka huu pekee kumekuwa na
ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari
ya Hindi karibu na nchini.
Kwa mujibu wa Pinda, jumla ya kilo 914 za Heroin zilikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia uharamia cha Jeshi la Kimataifa.
Alisema askrimu, mikate na maandazi
vilivyofanyiwa uchunguzi katika moja ya shule jijini Dar es Salaam
vilibainika kuwa na kiasi kidogo cha dawa hizo za kulevya.
Aliwataka walimu na walezi kuwa
makini na watu wanaouza vyakula katika maeneo karibu na shule ili
kuepuka wauzaji hao kuwafundisha wanafunzi kutumia dawa za kulevya.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment