ZIARA ya Rais wa Marekani, Barack Obama, imezidi kuwaweka njia panda
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, baada ya Serikali kuwataka wakazi wa
jiji hilo, ambao hawana shughuli muhimu, kutofika maeneo ya katikati ya
mjini kuanzia Jumamosi wiki hii.
Kauli ya Serikali, ilitolewa jana na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
wakati alikihojiwa na Redio Clouds FM, kuhusu manufaa ya ujio wa
viongozi wakubwa duniani nchini Tanzania.
Kutokana na hali hiyo,
Waziri Membe amewataka Watanzania ambao hawana shughuli za lazima katika
maeneo ya katikati ya jiji pamoja na eneo la Ubungo, kubaki nyumbani
muda wote ambao Rais Obama atakuwa nchini.
“Natumia fursa hii, kuwaomba Watanzania ambao hawana shughuli za
lazima katikati ya Jiji la Dar es Salaam wab
aki majumbani mwao, kwa
kipindi chote cha uwapo wa Rais Obama nchini,” alisema Membe.
Alisema
kutokana na mfumo wa ulinzi wa Marekani, kuna uwezekano mkubwa wa
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakazuiliwa kufika mjini na eneo la
Ubungo ambako Rais Obama atatembelea.
Kuhusu ziara hiyo, Waziri
Membe alisema: “Ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kuweza kujitangaza
kimataifa kwa kuvutia uwekezaji wa kiuchumi pamoja na utalii ambao
unaweza kuchangia pato kubwa la taifa.
“Nachukua fursa hii,
kuwaasa Watanzania wawe makini wakati dunia itakapokuwa hapa, tuwe
wavumilivu katika siku hizo mbili ili dunia iweze kuondoka salama katika
ardhi yetu ya Tanzania.
“Hii ni fursa ambayo ni adhimu sana,
kila Mtanzania anapaswa kuwa mlinzi, toeni taarifa pale mnapoona kuna
jambo lisilokuwa la kawaida, naomba tuionyeshe dunia kwamba sisi ni
wastaarabu, sitarajii kuwepo chokochoko za aina yoyote kwa kisingizio
chochote,” alisema Membe.
Hata hivyo, alipoulizwa, kwa nini
Serikali isitangaze siku ambayo Rais Obama atakuwa nchini kuwa siku
maalum ya mapumziko ili kuondoa mkanganyiko na usumbufu utakaojitokeza,
Membe alisema hilo si jukumu lake kulizungumzia.
Alisema kutokana
na ugeni huo mzito, Tanzania imetoa mwaliko kwa marais wote wa Jumuia
ya Afrika Mashariki kuja Tanzania kushiriki ziara ya Obama, lakini hadi
sasa hakuna aliyethibitisha.
Alipoulizwa kama Rais wa Rwanda,
Paul Kagame amealikwa, Waziri Membe alisema: “Ndiyo, Kagame amealikwa
kuja Tanzania kushiriki ziara hii ya kihistoria.
“Hili liko wazi,
tulitoa mwaliko tangu Februari, mwaka huu kwa marais wote wa Jumuiya
ya Afrika ya Mashariki kuja kushiriki nasi kumpokea Rais Obama, mpaka
sasa hatujapokea majibu rais gani atakuja, lakini tunawakaribisha hata
kwa dharura… nachukua fursa hii kutoa wito kwa Rais Kagame kama anaweza
kuja afike, tunamkaribisha sana,” alisema Membe.
Tanzania imepata
fursa ya kutembelewa na marais wawili wa taifa lenye nguvu zaidi
duniani. Mara ya kwanza Tanzania ilitembelewa na Rais mstaafu wa
Marekani, Bill Clinton, Agosti 28 hadi 29, 2000, akifuatiwa na Rais
mwingine mstaafu, George W. Bush, alitembelea Tanzania mwaka 2008.
Gari za usafi zatanda mjini
Wakati huo huo, makampuni ya usafi katikati ya Jiji la Dar es Salaam yamekuwa yakihaha kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Wengi wa wafanyakazi wa kampuni hizo, walionekana kuwa na vifaa vipya na mavazi nadhifu tofauti na siku zote.
Magari
ya usafi yameonekana kuwa mengi nyakati za mchana, huku yakikusanya
kila aina ya uchafu. Katika hali ya sasa hata maganda ya machungwa na
maji huwezi kuyaona.
POLISI
Idadi ya askari wanaofanya doria katika eneo la
katikati ya jiji na kandokando ya Barabara ya Nyerere ni kubwa kana
kwamba wanajiandaa kufanya operesheni maalumu.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambao wana silaha wamekuwa wakizunguka mitaa mbalimbali tofauti na siku zote.
KOVA ANENA
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam limejipanga kuimarisha ulinzi katika ziara ya
Obama na limezuia maandamano ya CUF ambayo waliomba kufanya Juni 29,
mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalamu ya Dar es Salaam,
Suleimani Kova, alisema barua ya CUF haikuambatanishwa na barua yoyote
kutoka Ikulu inayothibitisha kuwa Rais Jakaya Kikwete au wasaidizi wake,
wapo tayari kupokea maandamano hayo.
“Hatutaruhusu maandamano ya
aina yoyote, mabango, makundi yasiyokuwa na tija na aina yoyote ya
uvunjifu wa amani kwa kipindi hiki tutakapokuwa na ugeni katika nchi
yetu.
“Ni sifa kubwa kwa Taifa kama Tanzania kutumia fursa hii
kutangaza jina la nchi yetu katika mataifa mbalimbali duniani, endapo
tutadumisha amani, utulivu na ushirikiano wa hali na mali kwa wageni
wetu.
“Tunatarajia ziara ya kiserikali Julai 1-2 ya Rais Obama na
ujumbe wake, hivyo maandamano yao yataingilia maandalizi ya ziara hiyo,
hata hivyo barabara wanayotarajia kutumia, Buguruni Petrol Station
kupitia Barabara ya Uhuru ndiyo hiyo itaingiliana na misafara ya marais
14 na viongozi wakuu watakaokuja nchini katika mkutano wa Smart
Partnership Dialogue (SPD),” alisema Kamishna Kova.
Alisema Jeshi
la Polisi limepata taarifa za kuaminika kuwa kuna chama cha siasa na
taasisi ambazo zimejiandaa kusambaza vipeperushi au kujitokeza na
mabango ghafla barabarani wakati wa ujio wa Rais Obama wa Marekani,
kitendo ambacho ni kinyume cha taratibu za usalama. CHANZO MTANZANIA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment