Darfur, Sudan
HOFU imezidi kutanda mchini Sudan kutokana na mabigano makubwa yanayoendelea katika mji wa Darfur, hofu kubwa iliyotawala katika vichwa vya wanamichezo mbalimbali kutoka Afrika Mashariki na Kati ime
ongeza utata wa ushiriki wa timu katika Mashindano ya Kombe la Kagame.
Timu za Tanzania ambayo ndiyo inayotoa bingwa mtetezi wa Kombe hilo Young African Sport Club pamoja na Simba ambayo ni Bingwa wa Tanzania Bara mwaka jana, zilikuwa za kwanza kutangaza kwamba hazitashiriki katika mashindano hayo.
Hofu ya kutokwepo kwa mashindano hayo imeongezeka baada ya timu mbili kubwa nchini Sudan Al Hilal na Al Merreikhtimu kutangaza kuwa hazitashiriki katika michuano hiyo ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ikiwa yataandaliwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Uamuzi huo wa timu za Tanzania kutoshiriki mashindano hayo umechukuliwa kufuatia mjadala ulioibuka katika bunge la Tanzania baada ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard Membe kuhoji hali ya Usalama katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Adne Rage, amesema uongozi wa CECAFA ni sharti ubadilishe mahala pa fainali hizo la sivyo wao hawatashiriki. ''Hatuwezi kwenda Darfu kuvalia mavazi yasiyopenya risasi''.
Alisema Bwana Rage. ''Ni wazi kuwa hali ya usalama katika eneo hilo sio nzuri kama ilivyothibitishwa na serikali'' Aliongeza mwenyekiti huyo wa Simba.
Membe aliliambia bunge la Tanzania kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa kuandaa fainali hizo katika eneo la Darfur ambalo limekumbwa na mapigano ya mara kwa mara.
Membe amesema serikali ya Tanzania, inachunguza hali ilivyo na kuwa watachukua uamuzi muafaka kuhusiana na suala hilo.
''Hatuwezi kuwatuma vijana wetu katika eneo ambalo hatuna hakikisho la Usalama'' Alisema Membe.
Awali timu za Tanzania ambazo ndizo zenye ushawishi mkubwa wa mashabiki katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki yaani Mabingwa watetezi Yanga pamoja na Simba walikuwa wameonyesha nia ya kushiriki katika fainali hizo za Darfur ila wakapata hofu zaidi kutokana na kauli ya serikali ya nchi yao.
Hata hivyo Katibu mkuu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania (TFF), Angetile Osiah, amesema wao wamehakikishiwa usalama na eneo watakalopiga kambi wakati wa mashindano hayo.
Chanzo http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment