WATU WENGI WAZIRAI KATIKA MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA.
Editruda Mashimi,Dar es Salaam
UWANJA wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere umelipuka kwa vilio na majonzi mazito baada ya Mwili wa alieyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Marehemu Albert Mangwea kuwasili katika viwanja hivyo.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kupokea mwili wa msanii huyo uliow
asili katika viwanja hivyo majira ya saa 8:30 alasili.
Mwandishi wa Habarimpya.com aliyepiga kambi viwanjani hapo anaeleza kwamba kuna umati mkubwa wa watu kiasi cha kufunga shuguli zote za kijamii katika eneo hilo.
"Mwili wa Mangwea umewasili hapa jijini Dar es Salaam na kuna mati mkubwa sana hapa, watu wanalia watu wamechanganyikiwa kuona jeneza la marehemu, hivi tunavyozungumza kuna zaidi ya watu watatu wamezirai eneo hili"anasema Mwandishi wa Habarimpya.com.
Mapokezi ya Mwili wa marehemu ulitarajiwa mwishoni mwa wiki iliyopita lakini ikashindikana kutoka na sababu za kiusalama,pamoja na sababu za ushunguzi wa mwili wake uliyokuwa ukifanywa na jopo la Madaktari nchini Afrika Kusini.
CHANZ http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment