MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku
akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na
mashoga pamoja na watoto.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana
na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto
waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One
na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo
watakaojaa kwenye mazishi yake.
Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla
hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku
ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.
“Unajua kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,” alisema Aunty Lulu.

0 comments:
Post a Comment