WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya wa Tanzania Anne Makinda wametajwa kuhusika katika tukio la
kupigwa kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari.Nassari ambaye alipigwa na watu aliowaita kuwa ni wanachama wa CCM Juni 16 mwaka huu kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni Wilayani Mond
uli Mkoani Arusha alisema Makinda hampendi tangu alipoingia Bungeni.
Akizungumza na Habarimpya.com akiwa kwenye chumba
alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu
Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa anamchukia tangu alipomshinda
mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili
mwaka jana.
Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini
Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na
Green Guard wa CCM wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu
kura kwenye uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.
“Kipigo nilichopata Lowassa anahusika ananichukia, anataka urais lakini hawezi kuupata kwa kuuumiza watu kama hivi, alifikiri kwamba nitakufa sitakufa hadi kwa mapenzi ya Mungu, Makinda naye ananichukia na hapendi hata kuniona Bungeni” alisema, Nassari.

Alisema kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi
ambavyo kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna
yanayohusisha kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na
viongozi wa dini na siasa.
Nassari alidai akiwa kama wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo, alikumbana na mambo kadhaa yaliyomshangaza, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa jaribio la kutekwa mara mbili, kabla ya kushambuliwa kwa kipigo.

0 comments:
Post a Comment