BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NEWS ALERT:MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CHADEMA APATA DHAMANA.

Mkurugenzi wa ulinzi na usalalma taifa, Wilfred Lwakatare (katikati) akitetaja jambo na viongozi wa chama hicho, picha hii kutoka maktaba ya www.jumamtanda.blogspot.com

Editruda Mashimi,Dar es Salaam
HATIMAYE Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilfred Muganyizi Lwakatare aamepata dhamana na kurudi uraiani, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuam
ua kuwa dhamana yake iko wazi.

Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa katika viwanja vya Hahakama hiyo anasema kwamba, Lwakatare amepata dhama hiyo yenye dhamani ya tsh 10milioni pamoja na kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na kukabidhi hati za kusafiria Mahakamani hapo.

Awali Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kula njama na kupanga kumteka Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu. 

Hata hivyo, Mei 8, mwaka huu Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu aliwafutia mashtaka hayo matatu ya ugaidi na kuwabakizia shtaka moja linaloangukia kwenye jinai ya kula njama za kutenda kosa la kumdhuru Msacky kwa kutumia sumu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: