MAONI YA MHARIRI:

KATIKATI ya wiki hii, sanaa ya muziki ilipokea kwa huzuni
taarifa za kifo cha mwanamuziki Albert Mangwea aliyefariki nchini Afrika
Kusini alikokwenda kwa shughuli za muziki.
Marehemu Albert Mangwea.

Marehemu Albert Mangwea.

Bi Kidude playing in Nairobi, Kenya, in 2006.
KIFO cha Mangwea, msanii wa muziki wa Bongo Fleva
maarufu kama Ngwair kimekuja mwezi mmoja tangu kifo cha msanii mkongwe
na alama ya muziki wa mwambao, Bi Kidude.
Misiba hii mfululizo ni wazi imepoteza watu muhimu
katika sanaa ya muziki, ambao hakika walik
uwa sehemu ya mafanikio tunayoshuhudia kwenye fani hiyo kwa sasa.
uwa sehemu ya mafanikio tunayoshuhudia kwenye fani hiyo kwa sasa.
Kifo cha msanii Ngweair kimeacha maswali mengi
miongoni mwa wadau hasa kufuatia kutojulikana chanzo halisi cha kifo
chake kilichotokea katika mazingira ya utata.
Utata unakuja baada ya kuelezwa mengi kuhusu kifo
chake, ambacho kimehusishwa na ulevi wa pombe na matumizi ya dawa za
kulevya kupindukia.
Kulikuwa na taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao
ilieleza sababu ya kifo cha msanii, kwamba matumizi ya pombe, bangi na
dawa za kulevya ndiyo sababu ya kifo chake.
Ingawa taarifa hiyo haikuwa rasmi kwa maana ya
kuthibitishwa na familia ya marehemu, lakini hatunyimwi nafasi ya kuwapa
ushauri wasanii wetu, ambao wengi ni vijana wadogo kwa matumizi ya dawa
za kulevya.
Ni kawaida kusikia wasanii kujihusisha na vitendo
visivyokubalika mbele ya jamii, kwa mfano ulevi, uhuni, umalaya,
matumizi ya dawa za kulevya, bangi na mambo mengine yasiyofaa.
Namna yoyote ya kwenda kinyume na maadili
yanayokubalika mbele ya jamii, kunaweza kumchafua msanii ambaye anapaswa
kuwa alama ya kuelimisha na kukosoa kupitia sanaa ya muziki.
Lakini tunachokishuhudia kwa baadhi ya wasanii
wetu ni kwenda kinyume na mahitaji ya kuistawisha jamii kwa kujihusisha
na matendo mabaya yanayowachafua hata wao wenyewe.
Tuna ushahidi mkubwa jinsi wasanii
wanavyojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya, ulevi, bangi, umalaya
na uhuni. Matendo haya siyo tu yanamchafua msanii, bali pia hayana
mashiko mbele ya jamii.
Wasanii wanapaswa kutambua mchango wao katika
jamii na kuwa mfano wa kuigwa na siyo kinyume chake kama ambavyo
tumekuwa tukishuhudia katika fani ya muziki hapa nchini.

0 comments:
Post a Comment