Rais wa zamani na rais mweusi wa kwanza Afrika Kusini Nelson Mandela.
AFRIKA ya Kusini imesema afya ya rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela imeanza kuwa nzuri wakati jana akifikisha miaka 95 huju Rais Jacob Zuma akituma salamu za pongezi za siku ya kuzaliwa kwa Mandela katika taarifa na kueleza kuwa Afrika Kusini inajivuna kumwona kiongozi huyo mashuh
uri wa kimataifa ni wa kwao.
Mtoto wa kike wa Mandela Zindzi Mandela alithibitisha Alhamisi kwamba afya ya baba yake inaendelea kuwa nzuri. Anasema kuna wakati hali yake ilikuwa mbaya na ya kutisha , lakini wiki tatu zilizopita ameonyesha mabadiliko makubwa.
Anasema ana uhakika baba yake atarejea nyumba hivi karibuni. Kiongozi huyo mtetezi dhidi ya ubaguzi wa rangi amekuwa katika hospitali mjini Pretoria kwa zaidi ya mwezi mmoja akisumbuliwa na maambukizo kwenye mapafu.

0 comments:
Post a Comment