BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BARACK OBAMA KUTUA ARDHI YA TANZANIA SAA 8:20 MCHANA LEO.

Rais wa Marekani, Barack Obama anatua nchini kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni hatua yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.
 
Dar es Salaam. 
Yametimia! Baada ya siku kadhaa za kusubiri kwa hamu, vitabu vya historia ya Tanzania vinaongezewa kumbukumbu wakati Rais wa Marekani, Barack Obama atakapowasili nchini leo mchana kwa ziara ya siku mbili. 

Ndege ya Air Force One itakayombeba  Obama na msafara wake itakanyaga ardhi ya Tanzania saa 8.40 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambako atapokelewa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
 Obama ambaye anafuatana na mkewe Michelle na binti zake, Malia na Sasha, anatua Tanz
ania ikiwa ni sehemu yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.
Anawasili Tanzania akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda Ijumaa baada ya ziara yake ya Senegal.
Historia imetimia
Imepita miaka 50, tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipotembelea Marekani, Julai 13, 1963 na kukutana rais wa nchi hiyo wakati huo, John F Kennedy na ziara hiyo inaaminika kuanzisha urafiki wa viongozi hao ambao umedumu hadi sasa. 
Ujio wa Rais Obama una maana na faida kubwa kwa Tanzania katika maeneo ukiangalia kihistoria, kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi pia.
Ziara ya  Obama ni heshima kubwa kwa Tanzania na itaingia katika vitabu vya kihistoria kwani ana rekodi ya kuwa mtu mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuongoza taifa la Marekani. 

Kuchaguliwa kwake (Obama), ambaye baba yake mzazi alikuwa na asili ya Kenya kuliashiria nuru mpya kwa siasa za Marekani kwani watu weusi wa taifa hilo kwa miaka mingi walikuwa wakipigania haki za kufaidika na fursa za kiuchumi na kisiasa katika taifa la Marekani.
Tanzania, kwa miaka mingi ilikuwa inaunga mkono harakati za watu weusi na ndiyo maana iliikuwa karibu na viongozi wa harakati za kupigania haki za watu weusi.
Mwalimu Julius Nyerere alikuwa karibu na Martin Luther King na mkewe Correta , ambao waliongoza harakati za mtu mweusi kujikomboa.Pia, viongozi wengine wa harakati hizo za mtu mweusi kutambuliwa kule Marekani, Jesse Jackson, Andrew Young na Malcolm X waliitembelea Tanzania mara nyingi.    

Obama alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2008 alifurahiwa na wapenda amani kote duniani na hasa Waafrika kwani walimhesabu kuwa ni sehemu yao.
Kuja kwake leo ni heshima kubwa kwani Tanzania inakuwa nchi ya nne  Afrika kutembelewa na Obama baada ya Ghana mwaka 2009 na ziara yake ya hivi karibuni ya nchi za Senegal na Afrika Kusini.
Ukizingatia kuwa  Obama  ana miaka mitatu na nusu kabla ya kumaliza kipindi chake cha pili cha uongozi wake huenda ziara hii ndiyo ikawa ya mwisho kwake barani Afrika akiwa na wadhifa wa rais.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: